
Waziri
wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hussein Mwinyi akikata utepe kuzindua
vitabu vya mwongozo wa kutekeleza mfumo wa usimamizi wa ubora wa huduma
za maabara kitabibu vilivyoandikwa kwa lugha ya Kiswahili leo jijini
Dar es salaam. Kulia ni mkurugenzi wa washirika wa huduma za Afya
duniani (CLSI) Connie Adams.

Waziri
wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hussein Mwinyi akiowaonyesha wadau wa
huduma za afya nchini (hawapo pichani) moja ya kitabu cha mwongozo wa
kutekeleza mfumo wa usimamizi wa ubora wa huduma za maabara kitabibu
kilichoandikwa kwa lugha ya Kiswahili mara baada ya uzinduzi.
Wanaoshuhudia ni mkurugenzi wa washirika wa huduma za Afya duniani
(CLSI) Connie Adams (kulia) na Magreth Mhando, Mkurugenzi wa huduma za
Kinga wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii (kushoto).

Waziri
wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hussein Mwinyi akitoa ufafanuzi wa
masuala mbalimbali kuhusu sekta ya afya nchini mara baada ya kuzindua
vitabu vya mwongozo wa kutekeleza mfumo wa usimamizi wa ubora wa huduma
za maabara nchini.

Viongozi
wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii wakiongozwa na Waziri wa Afya na
Ustawi wa Jamii Dkt. Hussein Mwinyi wakiwa katika picha ya pamoja na
wadau wa sekta ya afya kutoka ndani na nje ya nchi leo jijini Dar es
salaam wakati wa uzinduzi wa vitabu vya mwongozo wa kutekeleza mfumo wa
usimamizi wa ubora wa huduma za maabara kitabibu.Picha na Aron Msigwa
–MAELEZO.