Friday, August 17, 2012

TTCL YATOA ZAWADI ZA IDD KWA VITUO VYA YATIMA DAR


Ofisa Mtendeaji Mkuu wa kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Said Amir Said akikabidhi zawadi za Sikukuu ya Idd kwa Sista, Mary Grisaldia na Mary Annie kwa ajili ya watoto wanaolelewa katika kituo cha watoto yatima cha Mama Teresa’s kilichopo Mburahati jijini Dar es Salaam.
Watoto wa Kituo cha kulelea yatima cha Msongola Kivule Kitunda jijini Dar es Salaam, Maria Daniel na Neema James wakipokea sehemu ya msaada wa vitu mbalimbali vilivyotolewa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Said Amir Said kwa ajili ya Sikukuu ya Idd.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Said Amir Said akiwa katika picha ya pamoja na walezi wa vituo vilivyopewa misaada pamoja na watoto.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Said Amir Said akifafanua jambo kabla ya kukabidhi msaada kwa vituo vya yatima.