Watu sita wamekufa na wengine arobaini na tatu kujeruhiwa mkoani Singida katika ajali mbili tofauti zilizo husisha basi la Nice Line kuligonga lori kwa nyuma na Noah iliyo kuwa ikienda kwenye msiba kupinduka.
Akithibitisha kutokea kwa vifoo hivyo mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Singida daktali Daniel Tarimo, amesema watu watano wamekufa katika ajali ya basi na moja amekufa katika ajali ya gari dogo aina ya Noha na wamepokea majeruhi arobaini na tatu wakiwa wamevunjika miguu na kulazimika wengine wanne kuondoa kabisa sehemu za miguu ambayo ilikuwa imesagika na kushindikana kuungwa.
Wakielezea baadhi ya abiria, majeruhi na mashuhuda wamesema dereva wa basi alikuwa katika mwendo wa kasi na kwakuwa ilikuwa usiku hakuweza kuyaona magari mawili yaliyokuwa yame haribika na alipoamua kukwepa gari moja alitoka nje ya barabara na kukanyaga kingo za baraba na kusababisha kuyumba na kuligonga lori lililokuwa limeegeshwa pembezoni mwa barabara likiwa bovu.
Akithibitisha kutokea kwa ajali hizo kamanda wa jeshi la polisi mkoani Singida ACP Thobias Sedoyeka amesema ajali zote mbili zimesababishwa na mwendo kasi pamoja na uzembe wa madereva kuto kuwa makini barabarani na mimehusisha basi la Nice Line lenye usajili wa namba T 174 CAV Scania lilokuwa likitoke Dar-es-Salaam na kueelekea Mwanza kuligonga roli namba RAT.317n/rl.o754 na ajali ya Noha yenye usali wa namba T.998 CWG iliyo kuwa ikitokea Dar-es-Salaam na kuelekea Kahama kwenye msiba.