Friday, August 17, 2012

Taswira Mbalimbali Kutoka Tume ya Mabadiliko ya Katiba

 Bi Joyce Kasambala (70) mkaziwaMpwapwamkoani Dodoma akisoma machapisho mbalimbali yanayotolewa naTume ya Mabadiliko ya Katiba wakati wa sherehe za Siku ya Wakulima Nanenane zilizofanyika hivi karibuni katika viwanja vya Nzunguni mjini Dodoma.
 Watoto hawa Saada Yusuph (7) kushoto na mwenzake Joseph Makwate (8) wa kata ya Nzunguni Manispaa ya Dodoma mjini wakisoma nakala za Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati walipotembelea banda la Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika sherehe ya siku ya Wakulima Nanenane zilizofanyika hivi karibuni katika viwanja vya Nzunguni mjini Dodoma.
Wakazi wa Manispaa ya mji wa Dodoma wakiwa katika foleni kusubiri kuingia katika Banda la Tume ya Mabadiliko ya Katiba wakati wa kilele cha siku ya Wakulima Nanenane zilizofanyika hivi karibuni katika viwanja vya Nzunguni mjini humo.
KatibuwaJukwaa la Wahariri(TEF) Neville Meenaakichangia hoja wakati wa mkutano wa kubadilisha na mawazo baina ya Uongozi wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba na Baraza la Habari Tanzania (MCT) pamoja na Jukwaa la Wahariri uliofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Warioba, Katibu waTume Assaa Rashid na Naibu Katibu Casmir Kyuki.Picha Zote na Tume ya Mabadiliko ya Katiba