Naibu
Waziri Wizara ya Nishati na Madini George Simbachawene (Mb)akizungumza
na wananchi wa kata ya Kaselya jimbo la Iramba Magharibi.
Naibu
Waziri Wizara ya Nishati na Madini George Simbachawene (wa kwanza
kulia) akisaini kitabu cha wageni cha ofisi ya kata ya Kaselya.
Na.Nathaniel Limu.
Serikali
imeahidi kuvipatia umeme wa grid vijiji 21 vya jimbo la Iramba
Magharibi na Iramba Mashariki ili pamoja na mambo mengine kuharakisha
upatikaji wa maendeleo endelevu.
Akizungumza
na wananchi wa kijiji cha Kaselya jimbo la Iramba Magharibi Naibu
Waziri wa Nishati na Madini George Simbachawene, amesema kati ya vijiji
hivyo, kijiji cha Msingi na Milade, ni vya jimbo la Iramba Mashariki na
vilivyobaki 19 ni vya jimbo la Iramba Magharibi.
Simbachawene
ametaja baadhi ya vijiji vya jimbo la Iramba Magharibi vitakavyonufaika
na mradi huo kuwa ni Kaselya, Mbelekese, Ndulungu, Malendi, Kitusha,
Lugwala, Moto moto, Kizaga, Kitukuntu, Kibigiri, New Kiomboi, Makunda na
Maluga.
Naibu
Waziri huyo amesema vijiji hivyo vitapata umeme kwa awamu tofauti,
lakini vijiji vya Mbelekese, Kaselya na Ndulungu, vitapata umeme katika
mwaka huu wa fedha utakaoishia juni mwakani.
Amesema kutokana na hatua hiyo, hivi sasa hakuna haja ya vijana kukimbilia mijini ambako hakuna kazi za kufanya.
Kwa
hali hiyo, amewataka wakazi wa vijijini, wasidhani kuwa umeme ni kwa
ajili ya kuwasha wakati wa kulala tu, umeme pia ni kwa ajili ya
maendeleo yao.
Naye
mbunge wa jimbo la Iramba Magharibi Mwigulu Lameck Nchemba, amewataka
wakazi wa maeneo yatakayopatiwa umeme, kutoa ushirikiano wa kutosha kwa
makandarasi watakaopewa kazi ya kusambaza umeme vijijini ili kazi hiyo
iweze kukamilika kwa haraka.