Takriban
watu 30 wameuawa nchini Afrika Kusini baada ya polisi kupambana na
kundi la waandamanaji wanaogoma ambao ni wafanyakazi wa mgodi wa
Marikana.
Kwa mujibu wa mashuhuda, polisi walifyatua risasi kwa waandamani hao waliokuwa wamebeba marungu na mapanga.
Mgodi
huo wa Platnum unaomilikiwa na Lonmin umewa kitovu cha vurugu za
malipo, uliochochewa na mvutano baina ya vyama viwili vya wafanyakazi.
Vurugu zilizokuwa zikiendelea wakati wa mgomo huo zilisha sababisha vifo vyatu 10.
Tukio hilo la polisi kumwaga damu za wananchi ni kubwa tangu kumalizika kwa ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini.