Timu
za waokoaji katika Mlima Kenya wamefanikiwa kupata miili minne ya
mwisho ya askari wa Jeshi la Ulinzi la Uganda waliopata ajali na
kuungulia ndani ya helkopta.
Jeshi
la Ulinzi la Kenya limesema miili hiyo imesafirishwa kuelekea Nairobi
kutoka eneo la tukio, na kukamilisha zoezi lililodumu kwa siku tatu la
kutafuta na kuoko.
Idadi
hiyi inafanya waliokufa katika ajali ya helkopta za Uganda zilizoanguka
katika maeneo ya Mlima Kenya nchini Kenya kuwa saba (7).