Mjumbe wa
Bodi ya Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) , Mariam Wilmore(kulia) ,
akimkabidhi hundi yenyethamani ya shilingi Milioni tatu kwa Diwani wa
Kata ya Somangila, Aisha Mpanjila (wapili kushoto), wengine ni Meneja wa
NHIF Kanda ya Temeke, Imelda Likoko, . Fedha hizo ni kwaajili ya
kusaidia ujenzi wa Zahanati ya Somangila Wilayani Temeke jijini Dar es
Salaam.
Diwani
wa Kata ya Somangila, Aisha Mpanjila (wapili kulia), akionesha hudindi
ya shilingi Milioni tatu aliyokabidhiwa na Mjumbe wa Bodi ya Mfuko wa
Bima ya Afya (NHIF), Mariam Wilmore(kulia) kwaajili ya kuchangia Ujenzi
wa Kituo cha Afya cha Somangila. Wengine ni Meneja wa NHIF Kanda ya
Temeke, Imelda Likoko (wapili kushoto) , na Meneja wa Masoko na Elimu
kwa Umma wa NHIF, Anjela Mziray.
---
Na Mwandishi Wetu
DIWANI wa Kata ya Somangila, iliyopo
Temeke, Aisha Mpanjila amesema kuwa kitendo cha Mfuko wa Taifa wa Bima
ya Afya cha kusaidia Zahanati ya Mbutu kitahamasisha wananchi wengine
kuchangia ujenzi unaoendelea katika zahanati hiyo na hatimaye kumaliza
tatizo la miundombinu.
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, jana ulikabidhi hundi yenye thamani ya
sh. Milioni tatu kwa lengo la kusaidia ujenzi wa wodi ya akina mama na
watoto.
Akipokea msaada huo, Diwani Mpanjila
alisema kuwa NHIF imeonesha njia na imekuwa mfano wa kuigwa hasa kwa
kutambua mahitaji ya wananchi katika sekta ya afya.
“Kweli nyie ni Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya…pamoja na kusaidia
wanachama wenu katika huduma za matibabu lakini mmekwenda mbali zaidi
kwa kutoa hata msaada wa kuboresha vituo vya kutolea huduma msaada ambao
unamgusa kila mtu…nawapongeza sana,” alisema.
Kutokana na hali hiyo, Diwani huyo alitumia fursa hiyo kuwaomba wananchi
wa maeneo hayo ambao ni wanufaika wa moja kwa moja na zahati hiyo
kuunga mkono Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kwa kuchangia ili ujenzi wa
wodi zilizopo zikamilike na zianze kutumika mara moja.
Naye Mjumbe wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Mariam Wilmore
amesema NHIF imeguswa na matatizo ya wakazi wa kata hiyo hivyo
itaendelae kusaidia kadiri ya uwezo wake.
Zahanati ya Mbutu inahudumiwa zaidi ya wakazi wa mitaa SITA inayozunguka kata hiyo.