Wednesday, July 11, 2012

HUKUMU YA BALOZI MAHALU YAAHIRISHWA



Balozi Mahalu (mwenye tai) akielekea kizimbani.
Grace Martin naye akielekea kizimbani kusikiliza hukumu yake.
Balozi Mahalu akitoka nje ya mahakama baada ya kesi yake kuahirishwa.
…Akifurahia jambo na wakili wake, Alex Mgongolwa (katikati), baada ya hukumu kuahirishwa.
Baadhi ya watu waliofika kusikiliza hukumu hiyo wakiwa nje ya mahakama hiyo.
Grace akiongea na ndugu zake baada ya hukumu kuahirishwa.
HUKUMU ya aliyekuwa balozi wa Tanzania nchini Italy, Costa Mahalu na Katibu Muhtasi wake, Grace Martin, katika kesi ya matumizi mabaya ya fedha, leo imekwama kutolewa kufuatia Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Kisutu Jijini Dar es Salaam, Ilvin Mgeta, aliyetakiwa kutoa hukumu hiyo kupatwa na udhuru.  Hivyo,  Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Aloyce Katemana, aliihairisha mpaka Agosti 9 mwaka huu.
                             PICHA : RICHARD BUKOS NA ISSA MNALLY / GPL