Wabunge wa CHADEMA Halima Mdee (Kawe)
ambaye anaonekana picha ya juu akiikataa keki hiyo iliyotolewa na
Wakurugenzi wa Nyumbani Longe, Gadna G Habash na Mkewe Lady Jay Dee,
huku Mbunge wa Viti Maalum, Lucy Kiwelu picha ya chini nae akijificha
asiitazame kwa karibu.
Wabunge hao waliigwaya Keki hiyo kutokana na jinsi ilivyopambwa rangi za CCM.
Huku Wabunge wa CCM wakishangilia wakimtaka Halima Mdee aongoze Ukataji wa Keki hiyo ambayo ilitolewa baada ya keki ya awali iliyoandaliwa na Baby Girl Shy Rose kuliwa, ilishindikana kuliwa na kuhifadhiwa.
Watu mbalimbali walihudhuria tafrija hiyo ndogo wakiwepo Wabunge, Wanasiasa, Wasanii wa Musiki, Watangazaji na Wanahabari ambapo kila aliye simama kuongea alimpongeza sana Shy Rose kwa kuwa Mpambanaji wa Ukweli katika kutafuta kile anachotaka na kumuombea kwa Mungu amuongoze vyema katika kazi yake.
CHANZO: FATHER KIDEVU BLOG