Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete
akihutubia katika ukumbi wa mikutano wa Brasilia Convention Centre
jijini Brasilia, Brazil, Aprili 17, 2012 katika mkutano wa Open
Government Partnership.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete
akilakiwa na mwenyeji wake Rais wa Brazil Mama Dilma Rousseff
alipowasili katika ukumbi wa mikutano wa Brasilia Convention Centre
jijini Brasilia, Brazil, Aprili 17, 2012 kuhudhuria mkutano wa Open
Government Partnership.
Ujumbe wa Tanzania kwenye mkutano wa
Open Government Partnership ukibadilishana mawazo kabla ya ufunguzi wa
mkutano huo katika ukumbi wa mikutano wa Brasilia Convention Centre
jijini Brasilia, Brazil, Aprili 17, 2012. Wa pili kutoka kushoto ni
Waziri katika ofisi ya Rais (Utawala Bora) Mh Mathias Chikawe, Waziri wa
Kazi na Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Ushirika wa Zanzibar Mh Haroun
Ali Suleiman, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Mh Mahadhi J. Maalim na Msahuri wa Rais (Masuala ya Siasa) Dkt Laurian
Ndumbaro.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa
meza kuu na mwenyeji wake Rais wa Brazil Mama Dilma Rousseff na wajumbe
wengine katika ukumbi wa mikutano wa Brasilia Convention Centre jijini
Brasilia, Brazil, Aprili 17, 2012 wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Open
Government Partnership. Kulia ni Waziri wa mambo ya Nje wa Marekani Bi
Hilary Clinton.
a7, a8 & a9: Wajumbe wa Tanzania
kutoka taasisi mbalimbali za kiraia na serikali wakiwa katika ukumbi wa
mikutano wa Brasilia Convention Centre jijini Brasilia, Brazil, April
17, 2012 wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Open Government Partnership.
a11: Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete
akiongea na Waziri Mkuu wa Georgie Mh Nika Gilauri katika ukumbi wa
mikutano wa Brasilia Convention Centre jijini Brasilia, Brazil, April
17, 2012 baada ya kuhudhuria mkutano wa Open Government Partnership
C1: Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete
akiongea na mabalozi wa nchi mbalimbali wakati wa Mchapalo ulioandaliwa
na Balozi wa Tanzania nchini Brazil Mh Francis Malambugi nyumbani kwa
Balozi usiku wa April 17, 2012 jijini Brasilia, Brazil
PICHA NA IKULU