Baadhi ya waombolezaji wakiwa nyumbani kwa marehemu.
Pichani juu ni badhii ya mashabiki wa
Kanumba waliopoteza fahamu na kudondoka chini baada ya kupata taarifa
za kifo chake cha ghafla.
Umati wa waombolezaji wakiwa nyumbani kwa marehemu Kanumba.
Mbuge wa Ubungo John Mnyika (Kushoto)
akisalimiana na Mkurugenzi wa Global Publishers Eric Shigongo, (Kulia)
ni ndugu Abdallah Mrisho.
Diwani wa Sinza Mr Simple (Kushoto) akiteta jambo na Mbunge wa Ubungo Mh: John Mnyika.
Mmoja wa Wakurugenzi wa Clouds FM, Ruge Mtahaba (aliyesimama) akimsikiliza Mhe:John Mnyika Mnyika.
Waombolezaji mbalimbali wakifarijiana kuhusu msiba wa kushitua wa Kanumba.
Msanii mahiri wa fialmu nchini tanzania
Steven Kanumba, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo baada ya kusukumwa
na mpenzi wake wakiwa nyumbani kwake Sinza jijini Dar es Salaam. Mpenzi
anayedaiwa kuwa nae amefahamika kwa jina la Lulu. Nyumbani kwa Marehemu
Kanumba kumefurika waombolezaji wengi sana ambao wamefika kuomboleza
msiba huo huku wengine wakija kuhakikisha kama habari ni za kweli.
(PICHA: Imelda Mtema, Erick Everist, Issa Mnally/GPL)
Kwa hisani ya GPL