Sunday, April 01, 2012

KILA LA KHERI UCHAGUZI ARUMERU


Naomba niwatakie kheri watanzania wote wa Arumeru ambao kwao leo wana uchaguzi wa mwakilishi wao Bungeni.

Nawaomba kila mwenye sifa ya kupiga kura aende Kituoni akapige kura. Baada ya kura rudi nyumbani kaa utulie subiri matokeo yatangazwe.

Msikubali kudanganywa kuleta vurugu wala mtafaruku na vyombo vya dola mtaumia bure.

Amani ya BWANA itawale shughuli nzima ya uchaguzi ili hata baada ya Uchaguzi huu Arumeru ibakie moja.