Tuesday, February 14, 2012

MBUNGE CHIKU ABWAO ANUSURIKA KUFA AJALI YA GARI






Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha Demokrasia na maendeo (Chadema) Chiku Abwao amenurika kifo baada ya gari lake lenye namba za usajili T 252 BSX VX ambalo alilokuwa akisafiria kutoka Dodoma kuja Iringa kukwanguliwa na fuso katika eneo la Doma mkoani Morogoro usiku wa leo

Akizungumza na Francis Godwin, leo mbunge huyo alisema kuwa lori hilo aina ya fuso lilimfuata upande wake na kumgonga na kuendelea na safari na kuwa bila umakini wa dereva wake hali ya usalama wake ulikuwa mdogo sana.

Kwani alisema kuwa lori hilo baada ya kukwangua upande wa dereva halikuweza kusimama liliendelea na safari na wao kupelekea taili la moja lilipasuka na kupelekea gari lao kuhama njia.

Hata hivyo alisema katika gari hilo walikuwa yeye na dereva wake na kuwa hakuna aliyejeruhiwa kutokana na kufunga mikanda na kuwa mikanda na mwendo mzuri wa dereva wake ndio umesaidia kupona katika ajali hiyo.
Chanzo: Jamii Forums