Tuesday, September 07, 2010

Memo Ofisini

Kutoka kwa: Utawala

Kwenda kwa: Wafanyakazi wote

Tarehe: Leo leo

Hatutopokea tena taarifa ya daktari kama kithibitisho cha kuumwa kwako. Kama umemudu kutembea hadi hospitali na kuonana na daktari, bila shaka unaweza kufika ofisini na kuchapa kazi.

Upasuaji umepigwa marufuku kuanzia hivi sasa. Kwa kuwa tulikuajiri ukiwa na viungo vyako vyote vya mwili, kufanya upasuaji wa kuondoa kiungo chochote kile kwenye mwili wako ni uvunjifu mkubwa wa mkataba wako wa ajira. Zingatia hilo.

Kila mfanyakazi anapewa siku 104 za kupumzika kwa mwaka, ambazo ni wikendi. Kifo siyo sababu ya kukosekana kazini. Hakikisha ratiba za mazishi ya ndugu, jamaa na marafiki unazipanga ndani ya siku hizo za kupumzika.

Endapo mfanyakazi yeyote ataaga dunia, atalazimika kutoa taarifa ya angalau wiki mbili kabla. Hilo ni muhimu sana ili aweze kumfundisha mtu mwingine wa kubadili nafasi yake.

Kwa kuwa kuna muda ambao hupotea kwa wafanyakazi kwenda msalani, sasa kutakuwa na zamu kwa kutumia utaratibu wa alfabeti za majina ya wafanyakazi. Wenye herufi A wataanza saa 2 kamili hadi na robo. Kisha watafuata wenye herufi B. Utaratibu huo utaendelea kwa kupokezana robo saa kwa kila alfabeti. Ikitokea hukubanwa haja wakati wa zamu ya alfabeti yako, utalazimika kusubiri zamu yako siku inayofuata. Ikitokea umebanwa kiasi cha kushindwa kujizuia, utabadilishana na mwenzako mwenye zamu kwa taarifa ya maandishi iliyosainiwa na mkuu wa kitengo angalau saa moja kabla ya kwenda msalani.

Pamoja tuchape kazi kwa juhudi na maarifa.

Kazi njema.

Utawala.