Sunday, February 22, 2015

Kimenuka Air Tanzania, Mamilioni Yatafunwa Kutokana na Ukodishaji ndege



Kimenuka Air Tanzania, Mamilioni Yatafunwa Kutokana na Ukodishaji ndege

Bodi ya Wakurugenzi ya shirika la ndege la taifa ATCL imemuamuru Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo Johnson Mfinanga kuwa simamisha kazi Mkurugenzi wa Fedha ajulikanaye kwa jina la Badru, Meneja wa Fedha Witness Mbaga, na kusimamisha mkataba wa cashier kwa uchotaji wa fedha za malipo ya kukodi ndege.

Mkurugenzi Mkuu aliye staafu mwezi huu wa February, alikodi ndege toka kampuni ya AVMAX ya Kenya bila kufuata taratibu za sheria ya manunuzi hivyo kujiwekea cha juu na kuandika hati ya malipo kwa kuwatumia watajwa hapo juu na kweda kuchukua pesa bank kwa pesa ya Kitanzania inayolingana na dollar elfu tano kila mwezi na wakati mwingine zaidi ya hapo kwa kipindi chote ndege hiyo ilipo kuwa ATCL.

Habari zaidi toka ndani ya shirika zina sema AVMAX wanadai kutopokea $55,000 kama sehemu ya malipo japo ndani ya shirika inasemekana pesa hiyo imelipwa na kupelekwa isipo julikana.