Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Utamaduni katika Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Bibi. Lily Beleko akiwahutubia wageni waalikwa wakiwemo Mapadre, Masista pamoja na Viongozi mbalimbali wakati wa Uzinduzi wa Kamusi ya Ukristo uliofanyika Baraza Katoliki la Maaskofu Tanzania (TEC) Kurasini Jijini Dar es Salaam 17 Agosti, 2016.
Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) Padre Ubadius Kidavuri akiwahutubia wageni waalikwa wakiwemo Mapadre, Masista pamoja na Viongozi mbalimbali wakati wa Uzinduzi wa Kamusi ya Ukristo uliofanyika Baraza Katoliki la Maaskofu Tanzania (TEC) Kurasini Jijini Dar es Salaam 17 Agosti, 2016.
Mwandishi wa Kamusi ya Ukristo, Padre Jorad Nyenyembe akiwahutubia wageni waalikwa wakiwemo Mapadre, Masista pamoja na Viongozi mbalimbali wakati wa Uzinduzi wa Kamusi ya Ukristo uliofanyika Baraza Katoliki la Maaskofu Tanzania (TEC) Kurasini Jijini Dar es Salaam 17 Agosti, 2016.
Katibu Mtendaji Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) Dkt. Selemani Sewangi akiwahutubia wageni waalikwa wakiwemo Mapadre, Masista pamoja na Viongozi mbalimbali wakati wa Uzinduzi wa Kamusi ya Ukristo uliofanyika Baraza Katoliki la Maaskofu Tanzania (TEC) Kurasini Jijini Dar es Salaam 17 Agosti, 2016.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Uchapishaji Vitabu ya Mkuki na Nyoka, Bw. Walter Bugoya akiwahutubia wageni waalikwa wakiwemo Mapadre, Masista pamoja na Viongozi mbalimbali wakati wa Uzinduzi wa Kamusi ya Ukristo uliofanyika Baraza Katoliki la Maaskofu Tanzania (TEC) Kurasini Jijini Dar es Salaam 17 Agosti, 2016.
Baadhi ya wageni waalikwa katika Hafla ya Uzinduzi wa Kamusi ya Ukristo wakifuatilia uwasilishwaji wa hotuba mbalimbali toka kwa Viongozi na Mgeni rasmi wa hafla hiyo 17 Agosti, 2016 Jijini Dar es Salaam.
(Picha/Habari na Benedict Liwenga-WHUSM).
Serikali imempongeza Mwandishi wa Kamusi ya Ukristo Padre Jordan Nyenyembe pamoja na wadau wengine waliohusika katika kufanikisha uandishi wa Kamusi hiyo.
Pongezi hizo zimetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Utamaduni katika Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Bibi. Lily Beleko ambaye alimwakilisha mgeni rasmi Mhe. Waziri Nape Nnauye wakati wa Hafla ya Uzinduzi wa Kamusi hiyo.
Akisoma hotuba kwa niaba ya Mhe. Waziri Nape Nnauye, Bibi. Beleko amesema kwamba Padre Jordan Nyenyembe anapongezwa kwa uandishi wa Kamusi hiyo kwani kunaonyesha juhudi za kukuza na kuitangaza lugha ya Kiswahili.
Alisema kwamba uandishi wa Kamusi ni kazi ngumu na endapo maneno ndani ya Kamusi hayatafsiriwi sawa sawa basi kuna uwezekano wa kusababisha chuki, ghasia na hata mapigano na hasa maneno yanayohusiana na masuala ya imani ya dini Fulani.
"Ni matumaini yangu kwamba, Kamusi hii itahamasisha na kurahisisha uelewa wa vitabu na maandiko mbalimbali kwa usahihi na ufasaha kwa jamii na kuleta upendo, utulivu na amani", alisema Beleko.
Aliongeza kuwa Wamisionari wa mwanzo wa imani ya kikristo walisaidia katika usahihishaji na uenezaji wa lugha ya Kiswahili kupitia vitabu na nyaraka mbalimbali, aidha walishiriki katika kuandika sarufi za Kiswahili, kamusi za kiswahili na kutafsiri Biblia kutoka lugha moja kwenda lugha nyingine hali ambayo ilisaidia kukuza dini ya Ukristo na kukuza lugha ya Kiswahili.
"Lugha yetu ya Kiswahili kila kukicha inazidi kukua na kupitia Kamusi hii tunaamini kwamba wasomaji wataongeza maarifa na ufasaha na kudumisha umoja, amani na uzalendo", alisema Beleko.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) Padre Ubadius Kidavuri ambaye aliliwakilisha Baraza hilo alieleza kwamba, ushirikiano kati ya serikali na taasisi za kidhni ni jhambo mhimu katika kusukuma maendeleo ya taifa.
"Katika Kanisa la Katoliki Tanzania linaunga mmkono jitihada zote za Wasomi na Wataalam wote wanaowezesha ujuzi na maarifa mbalimbali kidini na hata kielimu kuwafikia Wananchi katika kukabiliana na changamoto, hivyo nachukua nafasi kwa niaba ya Baraza, kumshukuru na kumpongeza Padre Jordan kwa jitigada zake za kubuni na kufanya kazi hii njema kwa Watanzania", alisema Padre Ubadius.
Naye Mwandishi wa Kamusi hiyo, Padre Jordan Nyenyembe alisema kwamba Kamusi hiyo inakamilisha kazi iliyoanza mwaka 2004 kama Makala katika Gazeti la Kiongozi iliyoitwa 'Kiswahili cha Mwanakanisa'.
Alisema kwamba, wasomaji watakaokuwa wanaitumia Kamusi hiyo wawe huru kumshirikisha kwa kutoa maoni yao mbalimbali ili aweze kuboresha katika matoleo yajayo.
"Mtakaoisoma Kamusi hii msisite kutoa maoni yenu ambayo yataniwezesha kuboresha katika matoleo yajayo", alisema Padre Jordan.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Uchapishaji Vitabu ya Mkuki na Nyoka, Bw. Walter Bugoya alieleza kwamba, kuandaa kamusi kama hiyo kunahitaji mtu kufahamu masuala mengi ambayo anatarajia kuyaandika, hivyo anakuwa na kazi kubwa ambayo inahitaji umakini, kutafuta maana sahihi ya maneno.
"Pia katikia suala la uhalili Mwandishi anahitaji kusaidiwa na Wahariri ili kazi yake iwe rahisi kwa wasomaji kwa kupata maana sahihi ya maneno ndani ya kitabu husika", alisema Bw. Bugoya.
Kwa upande wake Katibu Mtendaji Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) Dkt. Selemani Sewangi alisema kuwa, suala la lugha kwenye Makanisa ni muhimu sana kwani litasaidia kukuza uelewa wa mafundisho ya imani ya dini hiyo, hivyo amepongeza kazi ya uandishi wa Kamusi hiyo.