Taarifa iliyotukikia chumba chetu cha habari muda huu, inaeleza kuwa ajali mbali iliyohusisha mabasi mawili ya abiria, imetokea katika eneo la Manyoni Mkoani Singida na kupelekea vifo vya abiria 24 papo hapo na wengine kadhaa kujeruhiwa.
Akizungumza kwa njia ya kuelezea ajali hiyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, ACP Thobias Sedoyeka amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo iliyotokea majira ya saa nane mchana wa leo, ambayo inayahusisha mabasi ya Kampuni moja ya CITY BOYS ambalo moja lilikuwa likitoka Dar kwenda Kahama huku lingine likitoka Kahama kuelekea Dar. Taarifa kamili itawajia baadae kidogo.