Saturday, July 02, 2016

HESLB YAKANUSHA KUWA HAINA FEDHA



HESLB YAKANUSHA KUWA HAINA FEDHA

BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU



TAARIFA KWA UMMA

KUKANUSHA TAARIFA KWAMBA BODI HAINA FEDHA





Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inapenda kukanusha taarifa za upotoshaji zinazoenezwa kwa sasa kwamba haina fedha.

Si kweli kwamba Bodihaina fedha, ila ni kweli kwamba kumekuwa na ucheleweshaji wa kufikisha fedha za wanafunzi vyuoni kutokana na zoezi la kuhakiki wanafunzi wanaonufaika na mikopo linaloendelea vyuoni hivi sasa.

Hata hivyo, maandalizi ya malipo hayo yameshafanyika na 'pay sheets' zimeshapelekwa vyuoni tayari kwa wanafunzi wanaonufaika na mikopo kusaini.

Bodi inatarajia wakati wowote wiki ijayo baada ya zoezi la uhakiki kukamilika; itapeleka fedha hizo vyuoni.


IMETOLEWA NA:
KITENGO CHA HABARI, ELIMU NA MAWASILIANO
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
TAREHE 2 JULAI 2016