Friday, July 01, 2016

MWAMUZI BEJI YA FIFA ALAMBA NONDOZ LEO, ATUNIKIWA UWAKILI WA KUJITEGEMEA.



MWAMUZI BEJI YA FIFA ALAMBA NONDOZ LEO, ATUNIKIWA UWAKILI WA KUJITEGEMEA.
Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii

MWAMUZI msaidizi kutoka Tanzania mwenye beji ya Shirikisho la Soka duniani FIFA, Frank Komba amehitimu mafunzo yake ya sheria na kuapishwa kuwa wakili wa kujitegemea na Jaji Mkuu Othman Chande leo katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar es salaam. 

Komba ambaye ni mwamuzi wa kimataifa anaingia kwenye mlolongo wa wana michezo waliosomea sheria ambapo kwa anaamini hatua hii aliyofikia atatitumikia vizuri pia itamsaidia hasa katika kushughulikia vizuri masuala ya mpira pamoja na mambo mengine.

Akizungumza baada ya kuapishwa, Komba amesema kuwa ametimiza moja ya malengo yake lakini zaidi bado anahitaji kuendelea mbali na hapa halipo ila msingi mkubwa ni kuhakikisha anatendea haki hiki alichokipata kwa sasa. "Nina imani kutokana na kazi yangu nitaitumia vyema nafasi hii niliyokuwa nayo pia bado ninahitaji kuendelea mbele zaidi ya hapa,".

Komba amehitimu shahada yake ya uwakili mbali na hilo ni moja ya waamuzi wanaotegemewa na FIFA hapa nchini na ameshachezesha mechi mbalimbali za kimataifa na zaidi atasaidia kuinua mpira pamoja na kutumia nafasi yake kutoa ushauri kwa vyama vya michezo.

"Nitatumia nafasi yangu kutoa ushauri kwa vyama vya mpira na hata klabu pia kwani kumekuwa na sintofahami nyingi sana katika sheria za mpira,"amesema Komba.