Kwa niaba ya Bodi ya Wakurugenzi, Menejimenti na Wafanyakazi wote wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), Mkurugenzi Mkuu wa SUMATRA anasikitika kuufahamisha umma kuwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa SUMATRA Prof. Iddi S.N. Mkilaha (pichani) amefariki dunia ghafla usiku wa tarehe 24 Juni, 2014 Nyumbani kwake eneo la Boko, Dar es Salaam.
Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani
kwa Marehemu, Boko, Dar es Salaam.
Tunaomba tuungane na Familia ya Marehemu Prof. Mkilaha katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo ya msiba huu mkubwa.
Mkurugenzi Mkuu
SUMATRA
25 Juni, 2016