Shirika la Ndege la RwandAir hapa nchini linapenda kuwatangazia Watanzania wote na wasafiri wa Ndege zake, kuwa wamenza kufanya safari zake za anga katika miji 17 kwa nchi za Afrika Mashariki na kati likiwa na ndege kubwa nane.
Shirika hilo hivi karibuni, litaongeza ndege nyingine kubwa nne (mbili ni Airbus na mbili Boeing) na kufanya kuwa na jumla ya ndege kumi na mbili. Ndege hizo mpya zitaruka miji ya Mumbay, Guangzhou, Paris na London.
Hayo yamesemwa na Meneja Mkazi wa Shirika hilo hapa nchini, Ibrahim Bukenya. Pia anapenda kuwajurisha kuwa bei zao ni nafuu na hudumu nzuri kuanzi kukata tiketi hadi mwisho wa safari.