Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
SERIKALI imesema Wakala wa Umeme Vijijini (Rea) hategemei fedha kutoka Shirika la Maendeleo ya Milenia (MCC) katika usambazaji wa umeme vijijini.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ameyasema hayo leo wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari waliotaka kujua hatima ya Rea baada ya Marekani kupitia MCC kusitisha msaada huo.
Amesema kusitishwa kwa msaada wa Dola za Kimarekani milioni 472 hakutaathiri usambazaji wa umeme vijijini, kwa sababu serikali ilishatenga Sh. bilioni 940 zitakazosaidia upatikanaji wa umeme vijijini.
Profesa Muhongo amesema fedha zilizokuwa zinatolewa na MCC zilikuwa hazipelekwi Rea bali zilikuwa zinapelekwa katika miradi ya barabara, Maji na Umeme, lakini siyo kusaidia Rea kusambaza umeme.
Amesema Sh. bilioni 940 zimetengwa katika bajeti kwa ajili ya mradi wa Rea awamu ya pili, ikiwa na lengo la kufikia vijiji 2,500 pamoja na wateja 250,000 kuunganishwa.
Rea awamu ya pili itamalizika Juni 30, na Rea awamu ya tatu itaanza Julai mosi na itamalizika katika kipindi cha miaka miwili.
Waziri Muhongo amelitata Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kuwafuata wananchi vijijini wakiwa na fomu za kuwasajili kupata umeme.
Aidha aliwataka Tanesco kufungua ofisi ndogo vijijini kuliko kuishia katika ngazi za mkoa na wilaya.
Wazriri Muhongo ameitaka Tanesco na Rea kuhakikisha wanatumia transfoma zinazotengenezwa ndani kuliko zile za nje.
Amesema Transfoma zinaungua ovyo, wakandarasi mnatumia transfoma za nje na kuogopa za ndani kwa sababu ya gharama, tukikugundua tunakuachisha kazi.
Kuhusua kituo cha kuzalisha umeme cha Kinyerezi namba mbili kwa sasa kimeongeza uzalishaji na kufikia megawati 240, huku megawati 180 zikizalishwa kutumia umeme wa gesi na megawati 60 zikiwa ni umeme wa mafuta.
Mtanmbo wa kinyerezai namba moja kwa sasa unazalisha megawati 150.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akizungumza na wakala umeme vijijini (REA) pamoja na watendaji wa tanesco juu utoaji wa huduma kwa wananchi leo jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wakala umeme vijijini (REA) pamoja na watendaji wa tanesco wakimsikiliza Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (hayupo pichani)leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii)