Friday, April 01, 2016

MNYARWANDA ALIYE FARIKI KWENYE AJALI IRINGA AZIKWA MAKABURI YA MKANYAGENI



MNYARWANDA ALIYE FARIKI KWENYE AJALI IRINGA AZIKWA MAKABURI YA MKANYAGENI
leo (JANA)  31/03/2016  Mkuu wa wilaya Iringa ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa ameshiriki kwenye mazishi mazishi ya Mnywarwanda Jeannnete Mukashema aliyefariki kwenye ajali iliyotokea usiku Juzi. Bi Jeanette alikuwa akisafiri na mtoto wake ambaye naye aliumia kwenye ajali hiyo bado anaendelea na matibabu. 

Akizungumza Mh Kasesela alisema " Imeniuma sana kwani niliupokea mwili kwa mikono yangu tukiwa na waokoaji wengine alipo tolewa juu kwenye basi bado tukio hilo limo mawazoni mwangu na nguo zangu zikiwa na madoa ya damu , tulimpokea akiwa tayari amefariki. 

Kesho yake mtoto alipo zinduka akaanza kumtafuta mama yake nilipo mtembelea asubuhi, nilijua mama yake amekufa nilishindwa kumwambia leo alipo niona ameanza kulia amenikumbusha nikiwa miaka 11 nilipo ondokewa na mama yangu. lakini naamini yuko katika mikono salama, Mungu ni mwema baba yake na ndugu wengine wamekuj kutoka  Rwanda. BWANA AMETOA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE"