Saturday, April 16, 2016

MKE WA MTOTO WA MALKIA WA NORWAY AKUTANA NA VIJANA WALIOINGIA 5 BORA YA SHINDANO LA MASHUJAA WA KESHO LA STATOIL TANZANIA


MKE WA MTOTO WA MALKIA WA NORWAY AKUTANA NA VIJANA WALIOINGIA 5 BORA YA SHINDANO LA MASHUJAA WA KESHO LA STATOIL TANZANIA
Mke wa Mtoto wa Malkia wa Norway (Crown Princess of Norway), Mette Marit akifurahia jambo wakati alipokutana na kuzungumza na vijana watano waliongia katika hatua ya tano bora ya shindano la biashara la mashujaa wa kesho ambalo lina dhumuni la kuhamasisha ujasiriamali kwa mikoa ya kusini mwa Tanzania yaani Mtwara na Lindi, kwenye kambi yao iliyopo kwenye Jengo la Statoil ambao ndio wadhamini wa Shindano hilo, Masaki jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki. Kushoto kwake ni Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya Statoil Tanzania, Genevieve Kasanga.

Shindano la Mashujaa wa Kesho lilihusisha vijana wenye umri kati ya miaka 18 na 25 kutoka mikoa ya Mtwara na Lindi kuwasilisha mawazo yao ya biashara ambayo baadae yalibadilishwa na kuwekwa kwenye andiko la biashara.

Mwaka huu shindano hili lilivutia vijana zaidi ya 400 ambao waliwasilisha mawazo ya biashara zao zinazolenga sekta mbalimbali za uchumi kama kilimo, ufugaji, mawasiliano, na biashara nyingine ndogondogo. Vijana waliruhusiwa kushiriki mmoja mmoja au hata kuunda vikundi vya watu wawili mpaka watatu.
Mtoto wa Malkia wa Norway (Crown Princess of Norway), Mette Marit akisikiliza kwa makini maeneo ya namna shindano hilo lilivyoendeshwa kutoka kwa Afisa wa Kampuni ya Statoil Tanzania, Eric Mchome.
Mtoto wa Malkia wa Norway (Crown Princess of Norway), Mette Marit akipokea zawadi ya picha yenye mchoro wa wanyama aina ya Pundamilia, kutoka kwa Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya Statoil Tanzania, Genevieve Kasanga.
Mtoto wa Malkia wa Norway (Crown Princess of Norway), Mette Marit akiwa katika picha ya pamoja na Majaji wa shindano hilo.
 Mtoto wa Malkia wa Norway (Crown Princess of Norway), Mette Marit akiwa katika picha ya pamoja na Sehemu ya Washiriki hao.