Saturday, April 09, 2016

MCHEZAJI KANU WA NIGERIA AMBAYE NI BALOZI WA KAMPUNI YA STARTIMES ATOA MSAADA KWA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUMU WA SHULE YA MSINGI YA MAJI MATITU MBAGALA JIJINI DAR ES SALAAM


MCHEZAJI KANU WA NIGERIA AMBAYE NI BALOZI WA KAMPUNI YA STARTIMES ATOA MSAADA KWA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUMU WA SHULE YA MSINGI YA MAJI MATITU MBAGALA JIJINI DAR ES SALAAM
Mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Nigeria, Super Eagles, Nwankwo Kanu (wa pili kushoto), akitoka kusaini  kitabu cha wageni katika Shule ya Msingi ya Majimatitu baada ya kufika shuleni hapo leo asubuhi kutoa msaada kwa watoto wenye mahitaji maalumu wanao soma kwenye shule hiyo. Kushoto kwake ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Abdul Mgomi. Wengine ni walinzi wake.
Picha na habari na Dotto Mwaibale
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Maji Matitu Bw.  Abdul Mgomi akimkaribisha mchezaji huyo shuleni hapo. Kutoka kulia ni Mwalimu Shabani Msabaha wa shule hiyo, Mchezaji Kanu na Makamu Rais wa Kampuni ya StarTimes, Zuhura Hanif.
Mchezaji Kanu akizungumza katika hafla hiyo kabla ya kukabidhi msaada huo.
Hapa Kanu akimkabidhi msaada wa sabuni ya unga Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Abdul Mgomi.
Wanafunzi wenye mahitaji maalumu wa shule hiyo wakiwa kwenye hafla hiyo.
Wazazi wa watoto wa shule hiyo wakiwa kwenye hafla hiyo.
Kanu akitoa msaada wa magodoro.
Kanu akitoa msaada wa vyombo vya jikoni kwa wanafunzi hao.
Hapa Kanu akikabidhi unga wanafunzi hao. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha watoto hao, Rehema Lemway na kulia kwake ni Mlezi wa watoto hao, Somoe Said Omary.
Kanu akiwakabidhi wanafunzi hao Luninga.
Kanu akiwa katika picha ya pamoja na watoto hao.
Kanu akishiriki kucheza na watoto hao wakati wakitoa burudani.
Kanu akiwa katika picha ya pamoja na wazazi wa watoto hao.
Hapa Kanu akiwa katika picha ya pamoja na walimu wa shule hiyo.