Sunday, April 10, 2016

KIPINDUPINDU HAKIENEZWI KWA KUROGWA-WAZIRI UMMY MWALIMU



KIPINDUPINDU HAKIENEZWI KWA KUROGWA-WAZIRI UMMY MWALIMU
Na.catherine Sungura,Kyela 

Wananchi wa wilaya ya kyela wametakiwa kuachana na mila potofu na kupelekea kufanya mauaji ya watu kwa kuhusisha ugonjwa wa kipindupindu ni ugonjwa unaoletwa kwa imani ya kishirikina

Hayo yamesemwa leo na waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto Ummy Mwalimu,wakati alipofanya ziara katika wilaya hii na kuongea na watendaji wa halmashauri.

Mh.Ummy alisema ameshangazwa na baadhi ya wananchi katika kijiji cha unyakyusa kujichukulia sheria mkononi na kuwauwa wanawake watatu kwa madai ndio wanaoneza ugonjwa huo.

Naye mkuu wa wilaya ya kyela dkt. Thea Ntara alisema kamati yake ya ulinzi na usalama imeshawakamata watuhumiwa wawili wa tukio hilo na kuwafikisha mahakamani ingawa bado mtuhumiwa mmoja aliyekimbilia nchi jirani ya malawi anatafutwa.

Matukio hayo yametokea mwezi februari na machi mwaka huu.
Wilaya ya kyela ilipokea mgonjwa wa kipindupindu novemba 2015 na hadi kufikia machi 2016 jumla ya wagonjwa 405 waliugua ambapo vifo vilikua 8. Kwa sasa wilaya hii haina mgonjwa wa kipindupindu

Hali ya kipindupindu nchini imekua ni tatizo kubwa nchini,takribani mikoa yote tanzania bara imekubwa na ugonjwa huu tangu ulipotiwe mwezi agosti mwaka jana,isipokuwa kwa mkoa wa Ruvuma na Njombe ambapo hawajaripoti mgonjwa wowote hadi Sasa

Ripoti ya wizara ya afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto ya tarehe 4 machi mwaka huu inaonesha jumla ya wagonjwa 20,294 wametolewa taarifa na kati ya hao 320 wamepoteza maisha.Kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka,mwenendo wa kipindupindu unaashiria idadi ya wagonjwa nchini inaongezeka