Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC), Bi. Lolencia Bukwimba (Mbunge wa Busanda) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kukutana na kujadili taarifa za Kampuni ya Simu nchini (TTCL) leo jijini Dar es Salaam. Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC), Bi. Lolencia Bukwimba (hayupo pichani) katika mkutano na wanahabari leo jijini Dar es Salaam. Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC), Bi. Lolencia Bukwimba (Mbunge wa Busanda) akipitia nakala ya taarifa ya Kampuni ya Simu nchini (TTCL) jujiridhisha na takwimu zilizotolewa na taasisi hiyo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam.
KAMATI ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC) imeitaka Serikali kutekeleza kwa vitendo ahadi zake za kuiwezesha Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kujiendesha kibiashara. Akitoa maazimio ya Kamati ya PIC leo Dar es Salaam baada ya kukutana na kujadili taarifa za Kampuni ya Simu nchini TTCL, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya PIC, Bi. Lolencia Bukwimba (Mbunge wa Busanda) alisema, ili TTCL iweze kutekeleza jukumu lake kwa Taifa, Serikali iharakishe utekelezaji wa ahadi zake kwa Kampuni hiyo Kongwe ya Mawasiliano nchini. "Serikali ikamilishe kwa haraka mchakato wa kuondoka kwa Kampuni ya Bharti Airtel ndani ya TTCL, mchakato huu umechukua muda mrefu sana, ni vyema sasa ukatekelezwa sambamba na kuisaidia TTCL kupata malipo yake inayodai kutoka kwa Wateja wake zikiwemo taasisi za Serikali," alisema Bi. Bukwimba.
Aidha Mhe Bukwimba aliongeza kuwa, Kamati ya PIC inaiagiza Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kuharakisha mchakato wa kukabidhi Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kwa TTCL ili utumike kibiashara na kwa ufanisi zaidi kuliko hivi sasa ambapo umiliki wake haupo bayana. Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC), Bi. Lolencia Bukwimba (Mbunge wa Busanda) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kukutana na kujadili taarifa za Kampuni ya Simu nchini (TTCL) leo jijini Dar es Salaam.[/caption] Alisema kwa kipindi cha miaka 15 hivi sasa Serikali haijafanya uwekezaji wa aina yoyote ndani ya TTCL hivyo kuitaka kuwekeza ili kampuni iweze kusonga mbele kibiashara. "...Kwasababu huwezi kutegemea kupata mapato mazuri bila kuwekeza uwekezaji wa aina yoyote...miaka kumi na tano ni mingi mi nauhakika wakiwekeza fedha wataweza kuisaidia kampuni kuiuwisha na kuweza kufanya shughuli zake vizuri kama taasisi zingine.
." Agizo jingine la PIC kwa Serikali ni kuiongezea TTCL wigo wa kutumia rasilimali zake kama dhamana ili kupata mitaji kutoka taasisi za fedha na kufanikisha mpango wa kampuni hiyo wa kufanya mageuzi ya kibiashara. Awali, Wabunge waliochangia hoja katika kikao hicho, waliitaka Bodi na Menejimenti ya TTCL kusimamia kikamilifu mipango mizuri ya kibiashara iliyowasilishwa mbele ya Kamati. Wabunge Esther Matiko (Tarime Mjini), Steven Ngonyani (Korogwe) Riziki Lulida (Viti Maalum), Sabrina Sungura (Viti Maalum), na Frank Mwakajoka (Tunduma) wamesema, Seriki inao wajibu mkubwa wa kuisaidia TTCL ambayo kwa kipindi kirefu imekuwa ikipitia kipindi kigumu hasa kutokana na uwekezaji usio na tija uliofanywa ndani ya Kampuni hiyo.