Monday, April 25, 2016

DC HAPI ATEMBELEA UPANUZI WA BARABARA YA MWENGE-MOROCCO LEO.



DC HAPI ATEMBELEA UPANUZI WA BARABARA YA MWENGE-MOROCCO LEO.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Ally Salum Hapi leo ametembelea ujenzi unaoendelea wa upanuzi wa barabara ya Mwenge-Morocco kuona maendeleo yake. Barabara hiyo ambayo ilikua na kero kubwa ya foleni iliamriwa kupanuliwa na Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Magufuli katika hatua yake ya kubana matumizi na kupeleka fedha katika shughuli za maendeleo. 

Katika ziara yake hiyo Mh. Hapi alitembea umbali wa mita 500 kwa miguu kukagua pia usafi wa mazingira ya kando ya barabara ambapo alipofika katila kituo cha mafuta cha Total, aliagiza uongozi wa kituo kufanya usafi wa mazingira yaliyo mbele ya kituo chao.

Aidha Mh. Mkuu wa Wilaya pia alizungumza na Meneja wa TANROADS Mkoa wa Dar es salaam, Mkandarasi na wataalam wengine wa ujenzi na kujua maendeleo yao.

Meneja wa TANROADS na Mkandarasi walimueleza Mkuu wa wilaya kuwa tayari kazi imekamilika kwa asilimia 90 na kwa mbali wanatarajia kukabidhi mwezi June mwaka huu.
Mkuu wa Wilaya Kinondoni Mhe. Ally Hapi akikagua matengenezo ya barabara ya Ali Hassan Mwinyi leo tarehe 25 Aprili 2016 jijini Dar es Salaam
Mkuu wa wilaya Kinondoni Ally Salum Hapi wa kwanza kulia akipata maelezo kutoka kwa msimamizi wa ujenzi wa barabara ya Ali Hassani Mwinyi Halipo tembelea leo kuona maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo.
Mkuu wa Wilaya Kinondoni Mhe. Ally Hapi akiwa na wafanyakazi wa MS ESTIM CONSTRUCTION CO.LTD
Mkuu wa wilaya Mhe.Ally Hapi akiongea na msimamizi wa ujenzi.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Hapi kushoto akiwa na meneja wa Tanroad katika barabara ya Ali Hassan Mwinyi leo tarehe 25 Aprili 2016