Saturday, April 16, 2016

BONDIA IBRAHIMU CLASS 'KING CLASS MAWE' ASHINDA KWA POINT NCHINI PANAMA



BONDIA IBRAHIMU CLASS 'KING CLASS MAWE' ASHINDA KWA POINT NCHINI PANAMA
 Ibrahimu Class 'King Class Mawe'
 Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kulia akiwa na mpinzani wake Zapir Rasulov wa Russia baada ya kumshinda kwa point 
Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kulia akiwa na bondia Shane Mosley ambaye alishawai kucheza na Floyd Mayweather na kuonesha upinnzani mkubwa kushoto ni Rais wa ngumi za kulipwa nchini Emanuel Mlundwa hapa ni baada ya kushinda mpambano wake na Zapir Rasulov wa Russia kwa point.
 BONDIA Mtanzania Bingwa wa Afrika wa mikanda ya WPBF na U.B.O Afrika Ibrahimu Class 'King Class Mawe' april 15 mwezi huu amefanya maajabu baada ya kumtwanga bila huruma Bondia Zapir Rasulov wa Russia na kufanikiwa kumpiga kwa point katika mpambano uliofanyika katika ukumbi wa Hotel ya Convenciones Vasco nchini Panama City, Panama 
Class anakuwa bondia wa kwanza kumpiga bondia huyo katika mapambano yake 30 aliyocheza ambapo kati ya hayo mapambano 27 ameshinda kwa K.O na matatu kashinda kwa point
Bondia huyo alikuwa na rekodi ya kutopigwa hata mpambano mmoja  aliyocheza katika michezo yake yote na sasa Class ameweka doa katika michezo yake na kuwa bondia wa kwanza kutoka Afrika kumpiga bondia huyo anaesifika ugaibuni 
Bondia King Class Mawe baada ya kuibuka na ushindi huo amesema ushindi ni wa watanzania wote kwani yeye amekuwa mtumishi wao tangia mpambano wake wa kwanza ambao ulikuwa wa ubingwa alipokwenda nchini Zambia na kufanikiwa kumdunda bondia Mwansa Kabinga katika mpambano uliofanyika Arthur Davies Stadium, Kitwe, Zambia hii ilikuwa june 8 ,2014 na kushinda kwa TKO ya raundi ya tisa na kufanikiwa kurudi na mkanda wa WPBF Afrika
"Hivyo natarajia kuendeleza kuitumikia Tanzania na watu wake kupitia mchezo wa masumbwi nchini", amesema bondia huyo anaenolewa na jopo la makocha likiongozwa na kocha mkongwe kabisa Habibu Kinyogoli akisaidiwa na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' ambaye amekuwa akimshauri katika mapambano yake mblimbali nchini.
Bondia huyo anataraji kurudi nchini wakati wowote kwa ajili ya maandalizi ya mpambano mwingine wa masumbwi  hivi katibuni