Thursday, March 17, 2016

WAZIRI MKUU MAJALIWA AKIWA WILAYANI CHATO


WAZIRI MKUU MAJALIWA AKIWA WILAYANI CHATO
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa pole Joyce Thobias na mwanae Jonathan Mbarak ambaye amelazwa katika hospitali ya Wilaya ya Chato akimuuguza mwanae majeraha ya moto Machi 16,2916. mheshimiwa Majaliwa alikuwa katika siku ya kwanza ya ziara yake mkoani Geita.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasha gari la wagonjwa likiwa ni moja kati ya mawili yaliyotolewa msaada na Bibi Merete Trolle wa Denmark akisaidiwa kulisafilisha hadi hapa nchini na Mgodi wa Geita Gold Mine. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye hospitali ya wilaya ya Chato Machi 16, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua duka la dawa la MSD baada ya kulizindua kwenye hospitali ya wilaya ya Chato Machi 16, 2016. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya MSD, Profesa Mtulia.
Waziri Mkuu, Kasim Majaliiwa akihutubia mkutano wa hadhara mjini Chato , Machi 16, 2016.