Shirika la Ndege la RwandAir hapa nchini linapenda kuwafahamisha wasafiri wake kuelekea nchi za Rwanda na Kenya kuwa wanahitajika kuwa na vitabu vya chanjo (Yellow Fever) wakati wa safari.
Taarifa hizo nikutokana na maagizo kutoka Wizara za Afya ya nchi hizo mbili. Hata hivyo Meneja mkazi hapa nchini, Ndugu Ibrahim Bukenya anawaomba samahani wasafiri wote kwa usumbufu utakaojitokeza na kuwashukuru kwa kuchagua kusafiri na Shirika la RwandAir linalo toa huduma zake bora na zenye uhakika.