Wednesday, March 23, 2016

WANANCHI WA KATA YA NGURUKA WAHAMASISHWA KUJIUNGA MFUKO WA JAMII (CHF)



WANANCHI WA KATA YA NGURUKA WAHAMASISHWA KUJIUNGA MFUKO WA JAMII (CHF)
Na Editha Karlo wa blog ya jamii, Kigoma. 

MKUU wa Wilaya ya Uvinza,Mrisho Gambo amewataka Wananchi wa Tarafa ya nguruka kuchangia Mfuko wa afya ya jamii (CHF) ili kuwa na uhakika wa matibabu pale wanapougua wao na familia zao.

Hayo ameyasema  katika Mkutano wa hadhara wa kuzindua kampeni ya uhamasishaji wa  kuchangia mfuko CHF katika kata ya Nguruka  uliofanyika jana kwenye viwanja vya shule ya msingi Nguruka.

Gambo alisema kuwa katika hospitali ya Nguruka kuna changamoto kubwa ya upungufu wa dawa kutokana na hali hiyo aliwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kuchangia mfuko huo iliwaweze kuwa na uhakika wa  kupata dawa na matibabu matibabu mengine katika hospital yao.

"Ninawaomba ndugu  zangu changieni CHF ili muwe na uhakika wa matibabu mnapo umwa tambueni ugonjwa unapokuja huwa hauna taarifa unaweza kuumwa na mfukoni huna pesa lakini kama umechangia CHF utakuwa na uhakika wa matibabu"alisema Mkuu huyo wa Wilaya.

Alisema uongozi wa Wilaya ya uvinza una mpango wa kukiboresha kituo cha afya cha Nguruka  kutokana na ahadi ya Muheshimiwa Rais wakati wa kampeni kukifanya kituo hicho kuwa Hospitali ya Wilaya na maandalizi yanaendelea.

Naye Mkurugenzi wa mifuko ya jamii(CHF) kutoka makao makuu ya bima ya afya (NHIF) Eugen Mikongoti aliwataka wananchi kuchangia mfuko huo kwa wingi kwakuwa serekali nayo uwachangia kiasi kile kile walichochangia wao ambayo huitwa tele kwa tele.

Mikongoti alisema endapo wananchi watachangia kwa wingi na hudumaza afya  zitaboreshwa zaidi kituoni hapo. "Nataka niwaambie hivi sisi wote ni wagonjwa watarajiwa, hakuna anayejua atagua lini tunachotakiwa ni kujiandaa kwa kujiunga na CHF ili tuwe na uhakika wa matibabu tutakapi ugua"alisema Mikongoti

Kwa upande wake Meneja wa bima ya afya Mkoa wa Kigoma Elias Odhiambo alisema kuwa hali ya uchangiaji wa mfuko wa afya ya jamii kwa kata ya nguruka hairidhishi hivyo kushindwa kufikia malengo ya huduma za afya.

Alisema kata ya Nguruka ina jumla ya kaya 6000 lakini kaya 756 ndiyo zimejiunga na kuchangia CHF.

"Kutokana na uhamasishaji wa kujiunga na CHF tuliofanya leo hapa jumla ya kaya 868 zimejiunga na mfuko huo hapa hapa, kwakweli ni jambo zuri sana tuendelee kujiunga kwaajili ya uhakika wa matibabu pale tunapougua.
Mkuu wa Wilaya ya uvinza Mrisho Gambo akiwahamasisha wananchi wa kata ya Nguruka kujiunga na mfuko wa afya ya jamii(CHF) kwenye uzinduzi uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Nguruka
Mkurugenzi wa mifuko ya jamii kutoka makao makuu ya bima ya afya Eugen Mikongoti akiwahamasisha wananchi wa Nguruka kujiunga na mfuko huo.

Vikundi vya burudani vikitumbuiza wakati wa uzinduzi wa uhamasishaji wananchi kujiunga na mfuko wa afya ya jamii kata ya Nguruka.


Baadhi ya umati wa wananchi waliojitokeza katika uzinduzi wa kuhamasisha kujiunga na mfuko wa afya ya jamii CHF kata ya Nguruka
Mkurugenzi wa mifuko ya jamii Eugin Mikongoti(mwenye koti jeusi) akiteta jambo na Meneja wa mfuko wa bima ya afya wa Mkoa wa Kigoma Elias Odhiambo wakati wa uzinduzi wa uhamasishaji wananchi kujiunga na CHF kata ya Nguruka