Friday, March 18, 2016

WAANDISHI WA HABARI KUTOKA NCHINI FINLAND WATEMBELEA TAASISI YA UONGOZI.


WAANDISHI WA HABARI KUTOKA NCHINI FINLAND WATEMBELEA TAASISI YA UONGOZI.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya UONGOZI Profesa Joseph Semboja (wapili kutoka kushoto) akizungumza na kundi la waandishi wa habari kutoka nchini Finland (hawapo pichani) mapema leo walipotembelea taasisi hiyo. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Idara ya Ushirikiano katika Ubalozi wa Finland nchini Tanzania Bi. Milma Kuttenen, Mshauri wa masuala ya Ushirikiano kutoka Taasisi ya UONGOZI Bi. Liisa Tervo na Mkuu wa Utafiti na Sera kutoka Taasisi ya UONGOZI Bw. Dennis Rweyemamu. 
 Kundi la waandishi wa habari 15 kutoka nchini Finland waliotembelea Taasisi ya UONGOZI mapema leo ikiwa ni moja kati ya mafunzo yao katika programu maalum ya maendeleo na sera inayoratibiwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Finland. Waandishi hao ambao wapo nchini kwa muda wa siku tano pia walisindikizwa na watumishi wawili kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Finland.
 Mratibu wa programu ya Maliasili Bi. Namwaka Omari (kulia) akitoa mada kwa waandishi hao wa habari kuhusu namna Taasisi ya UONGOZI inachangia katika kuimarisha usimamizi wa maliasili zetu nchini hususan katika sekta ya mafuta na gesi.
 Mmoja kati ya waandishi hao akiuliza swali. Baadhi ya mada zilizogusiwa katika mazungumzo ni pamoja na jinsi gani Tanzania inatekeleza dhana ya maendeleo endelevu, uimarishaji wa uwezo kwa viongozi barani Afrika, uchumi wa sekta ya gesi nchini na utekelezaji wa majukumu ya Taasisi ya UONGOZI katika mazingira ya Serikali Mpya.
Mkuu wa Idara ya Ushirikiano katika Ubalozi wa Finland nchini Tanzania Bi. Milma Kuttenen (kushoto) akitoa neno lake la shukrani kwa niaba ya waandishi wa habari na maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Finland, walipotembelea Taasisi ya UONGOZI kufahamu shughuli zake mapema leo.