Saturday, March 19, 2016

WA ADVENTISTA WASABATO WAADHIMISHA SIKU YA MATENDO YA HURUMA KWA KUCHANGIA DAMU LEO



WA ADVENTISTA WASABATO WAADHIMISHA SIKU YA MATENDO YA HURUMA KWA KUCHANGIA DAMU LEO
 Mgeni Rasmi katika maadhimisho Mkuu wa mkoa wa dar-es-salaam Mhe. Paul makonda akihutubia waumini waliojitokeza changia damu
 Wageni waalikwa katika maadhimisho hayo kutoka kushoto Meneja damu salama kanda ya Mashariki Dr Aveline Mgasa,  Mganga mkuu mkoa wa Dar , Dr Grace magembe, Mhe. Paul Makonda, Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dr Mpoki Ulisubya.
Baadhi ya waumini wakichangia damu kwa hiari

Mpango wa Taifa wa Damu salama kwa kushirikiana na waumini wa dhehebu la sabato wameendesha zoezi la kuchangia damu katika mikoa mbalimbali hapa nchini, mikoa hiyo ni Mara, Kigoma, Dar-es-salaam, Dodoma, Mwanza, Kilimanjaro,Tabora, Morogoro, Mbeya na Iringa.

Siku ya matendo ya huruma hufanyika jumamosi ya tatu ya mwezi wa tatu kila mwaka, ambapo waumini hushiriki katika huduma mbalimbali za jamii. Lengo ni kukusanya chupa za damu 3000 kutoka katika mikoa hiyo ambazo zitasambazwa Hospitali mbali mbali kuokoa maisha ya wahitaji