Saturday, March 19, 2016

UMOJA WA WALIOSOMA KIGOMA SEKONDARI MWAKA 1991 -1994 WAZINDULIWA


UMOJA WA WALIOSOMA KIGOMA SEKONDARI MWAKA 1991 -1994 WAZINDULIWA

Mwenyekiti wa Umoja wa Waliosoma Shule ya Sekondari Kigoma mwaka 1991 – 1994 (UWKS) Dkt. Nelson Boniface akizungumza wakati wa mkutano mkuu wa kwanza wa Umoja huo uliofanyika leo katika ukumbi wa Golden Tulip Hotel jijini Dar es Salaam.
Katibu Msaidizi na Msemaji wa Umoja wa Waliosoma Shule ya Sekondari Kigoma mwaka 1991 – 1994 (UWKS) Bibi. Elizabeth Bisendo akifafanua jambo wakati wa mkutano mkuu wa kwanza wa Umoja huo uliofanyika leo katika ukumbi wa Golden Tulip Hotel jijini Dar es Salaam.
Mwanasheria na Mratibu wa Umoja wa Waliosoma Shule ya Sekondari Kigoma mwaka 1991 – 1994 (UWKS) Wakili Msomi Marko Anthony Nsimba akielezea namna alivyoshughulikia suala la usajili wa Umoja huo wakati wa mkutano mkuu wa kwanza wa Umoja huo uliofanyika leo katika ukumbi wa Golden Tulip Hotel jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanachama wa Umoja wa Waliosoma Shule ya Sekondari Kigoma mwaka 1991 – 1994 (UWKS) wakiwa katika mkutano mkuu wa kwanza wa Umoja huo tokea kuanzishwa kwake mnamo mwaka 2011.
Baadhi ya wanachama wa Umoja wa Waliosoma Shule ya Sekondari Kigoma mwaka 1991 – 1994 (UWKS) wakiwa katika mkutano mkuu wa kwanza wa Umoja huo tokea kuanzishwa kwake mnamo mwaka 2011.
Mwanasheria na Mratibu wa Umoja wa Waliosoma Shule ya Sekondari Kigoma mwaka 1991 – 1994 (UWKS) Wakili Msomi Marko Anthony Nsimba akikabidhi Cheti cha usajili kwa Mwenyekiti wa Umoja huo Dkt. Nelson Boniface wakati wa mkutano mkuu wa kwanza wa Umoja huo uliofanyika jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia ni Katibu Msaidizi Bibi. Elizabeth Bisendo na Katibu Mkuu Godwin Ndaki.
Mwenyekiti wa Umoja wa Waliosoma Shule ya Sekondari Kigoma mwaka 1991 – 1994 (UWKS) Dkt. Nelson Boniface akionyesha Cheti cha Usajili wa Umoja wao mara baada ya kukabidhiwa na Mwanasheria na Mratibu wa Umoja huo Wakili Msomi Marko Anthony Nsimba (hayupo pichani) leo jijini Dar es Salaam.Kutoka kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa UWKS Janti Benjamini, Katibu Mkuu Dkt. Godwin Ndeki na Kati Msaidizi Bibi. Elizabeth Bisendo.
Mwenyekiti wa Umoja wa Waliosoma Shule ya Sekondari Kigoma mwaka 1991 – 1994 (UWKS) Dkt. Nelson Boniface akipitia Katiba iliyosajiliwa ya Umoja wao mara baada ya kukabidhiwa na Mwanasheria na Mratibu wa Umoja huo

UWKS 1991-94 yazinduliwa

Na: Mwandioshi Wetu.

Umoja wa waliosoma shule ya sekondari Kigoma mwaka 1991-1994 umezinduliwa leo rasmi baada ya mwanasheria wao Wakili Marko Anthony Nsimba kukabidhi cheti cha kusajiliwa na katiba ya umoja huo kwa wanaumoja huo hii leo.

Akizungumza baada ya kupokea cheti hicho, Mwenyekiti wa Umoja huo kwa niaba ya wanachama Dk Nelson Boniface amesema, lengo kuu la UWKS kuwakutanisha pamoja wanafunzi waliosoma Shule hiyo kuanzia 1991-94. Boniface ameongeza kuwa pamoja na kukutana, lakini pia nikusaidiana katika shida na raha kushiriki katika mambo mbalimbali ya maendeleo katika taifa letu sambamba na kutoa ushauri, michango ya misaada ya hali na mali kwa jamii yenye uhitaji.

Aidha umoja utashirikiana na taasisi mbalimbali za Kiserikali na zisizo za Kiserikali katika maendeleo ya jamii ya watanzania. Wakati huohuo amezitaja baadhi ya changamoto ambazo umoja huo umekutana nazo ikiwa ni pamoja na baadhi wahitimu wenzao kutoamini kuwa wanaweza kuwa na umoja na wengine wakithubutu kusema ni kupoteza muda.

"pamoja na kupotezana kwa Zaidi ya miaka 20 iliyopita, lakini sasa tumeweza kukutana tena ingawaje siyo wote laakini kwa kuwa lengo letu ni moja tuna amini na wengine watakuja taratibu" amesema . Mmoja wa wajumbe wa UWKS Mbunge wa Kigoma Mjini Zito Kabwe(ATC) amesema tuliopo ni wajumbe 18, imefanyika kazi kubwa kutafutana lakini naamini kila mmoja wetu atabeba jukumu la kuwavuta wengine hadi darasa litatimia.

Kabwe ambaye ni ameweka wazi kuwa Umoja huo utapeleka msaada katika shule hiyo kwa kuwa imechakaa na kurekebisha baadhi ya miundombinu iliyochakaa kwa kuwa wakati wao wakisoma walikuta maabara zikifanya kazi lakini kwa sasa zimechakaa, hiyo ni kama kurudisha shukrani kwa jamii.

Umoja wa Waliosoma Shule ya Sekondari Kigoma kuanzia 1991 -1994 (UWKS) umetokana na kikao cha wanajumuiya cha tarehe 06 Machi 2011ambapo ndipo lilipopatikana wazo la kuwa na Umoja huu ndipo wajumbe walipo azmia kuanza mchakato wa kusajili Umoja huo ambao leo umezinduliwa rasmi. Wajumbe waliojiorodhesha idadi yao inafikia 40 mapaka sasa.