Mmoja wa wagombea Urais kwa tiketi ya chama cha TLP Bwana. Hafidh Hassan Suleiman akithibitika wa kugombea na kuwataka wananchi kumpikia kura yeye. Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.
Na waandishi wetu. Maelezo Zanzibar.
Umoja wa vyama vya siasa ambavyo havina uwakilishi Bungeni wametoa tamko rasmi la kushiriki uchaguzi wa marejeo tarehe 20 mwezi huu na wamewataka wazanzibar kujitokeza kwa wingi kwenye uchaguzi huo.
Hayo yamezungumzwa na makatibu wakuu wa vyama hivyo wakati walipokuwa wakizungumzwa na waandishi wa habari katika ukumbi wa studio za Rahaleo mjini Zanzibar.
Wamesema Chama chochote cha siasa kazi yake ni kushiriki uchaguzi na sio kususia kwani kufanya hivyo kutakoseshawananchi haki yao ya msingi na kurudisha nyuma shughuli za maendeleo.
Aidha wameamua kurejea uchaguzi huo kutokana na kasoro zilizojitokeza uchaguzi wa mwanzo ambapo mambo mengi yalionesha dhahiri ulikuwa na kasoro za wazi wazi.
Makatibu hao wamesema kurejewa uchaguzi sio jambo geni duniani na yapo mataifa mengi yamewahi kurejea uchaguzi kutokana na kasoro mbali mbali zilizojitokeza katika chaguzi zao.
Viongozi wa Umoja huo wamesema pamoja na kushiriki uchaguzi pia wamesimamisha wagombea 12 ambao wamo katika ngazi zote ikiwemo rais, wawakilishi na madiwani.
Mwenyekiti wa umoja huo Ali Kaniki amewataka wazanzibari kujitambua na kufikra kwani wakiweza kujitambua wataweza kutoa maamuzi yaliyo sahihi.
"Wazanzibar tujitambue kifikra kwani tukiwa tunajitambua tutaweza kutoa maamuzi yalio sahihi, alisema Kaniki"
Kwa Upande wake mjumbe wa umoja huo Abdul Mhuya amesema khatma ya wazanzibar imo mikononi mwa wazanzibar wenyewe na Tanzania kwa ujumla hivyo wazanzibar wasikubali kuuipoteza thamani yaoya kushiriki kupiga kura kwa kupata viongozi wawatakao.
Vyama vitakavyoshiriki katika marudiao ya uchaguzi huo ni DP,CCK, AFP, DEMOKRASIA MAKINI , SAU, TLP, UPDP, UMD, ADC, NRA, TADEA NA CHAUMMA.