Tuesday, March 29, 2016

TAMASHA LA PASAKA LAHITIMISHWA MJINI KAHAMA MKOA WA SHINYANGA



TAMASHA LA PASAKA LAHITIMISHWA MJINI KAHAMA MKOA WA SHINYANGA
23
Mkurugenzi wa Utawala Wizara ya Ujenzi na Mawasiliano Bi. Katolina Kipa Mgeni rasmi wa Tamasha la Pasaka ambaye alimwakilisha Waziri wa Ujenzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akisoma hotuba kwa niaba ya waziri Profesa Mbarawa katika tamasha hilo kushoto ni Alex Msama wa pili kutoka kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kahama Mh. Vita Kawawa na Mbunge wa jimbo la Kahama Mh. Jumanne Kishimba.24
Mwimbaji Upendo Nkone akiwaimbisha mashabiki wake wakati alipokuwa akitumbuiza jukwaani kwenye uwanja wa Taifa mjini Kahama.
kwaani huku mashabiki wakicheza kwa furaha.
18
Mashabiki wakicheza kwa furaha katika tamasha hilo lililofanyika kwenye uwanja wa Taifa mjini Kahama.
25
Mwimbaji Boniface Mwaiteje na Faustine Munishi kutoka nchini Kenya wakifanya mambo makubwa jukwaani kama wanavyoonekana.

5
Mkurugenzi wa Msama Promotion Bw. Alex Msama akisalimiana na Bw. James Lembeli wakati alipokuwa akipmokea kwenye uwanja wa Taifa mjini Kahama leo.
2
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akimpokea Mkurugenzi wa Utawala Wizara ya Ujenzi na Mawasiliano Bi. Katolina Kipa Mgeni rasmi wa Tamasha la Pasaka ambaye alimwakilisha Waziri wa Ujenzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa katika tamasha hilo lililofanyika kwenye uwanja wa Taifa mjini Kahama leo na kuhudhuriwa na Mkuu wa wilaya ya Kahama Mh. Vita Kawawa, Mbunge wa jimbo la Kahama Mh. Jumanne Kishimba na aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo hilo Ndugu James Lembeli.

Waimbaji mbalimbali wametumbuiza katika tamasha hilo ambalo ndilo limehitimisha matamasha ya pasaka ya mwaka huu yaliyofanyika katika mikoa ya Geita , Mwanza na Shinyanga katika kanda ya ziwa, Waimbaji hao ni Upendo Nkone, Jennifer Mgendi, Boniface Mwaiteje, Martha Baraka, Goodluck Gozbert , Jesca BM, Christopher Mwahangila, Ephraim Sekereti na wengine wengi. (PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-KAHAMA)