Mkurugenzi wa Hospitali ya Walemavu CCBRT, Bi. Brenda Msangi akimueleza Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai (kulia) kuhusu namna ya utendaji kazi hospitalini hapo. Spika alitembelea hospitali hiyo kuangalia utendaji kazi kama mlezi wao.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (mwenye tai nyekundu) akipokea machapisho yanayohusu masuala ya walemavu kutoka kwa Afisa Mtetezi CCBRT wa masuala ya walemavu, Bw. Fredrick Msigala wakati alipotembelea hospitali hiyo kwa mara ya kwanza akiwa ni Mlezi wa Hospitali hiyo.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (wa pili kulia) akipata maelekezo juu ya namna ya wagonjwa wa macho wanavyowekewa macho bandia (artificial eyes) wakati alipotembelea hospitali hiyo kwa mara ya kwanza akiwa ni Mlezi wa Hospitali hiyo. Kulia ni ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mpoki Ulisubisya.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muunganao wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai (kulia) akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya CCBRT Bw. Erwin Telemans (kushoto) wakati alipotembelea hospitali hiyo kwa mara ya kwanza akiwa ni Mlezi wa Hospitali hiyo.Katikati ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mpoki Ulisubisya.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Wizara ya Afya nchini pamoja na Menejimenti ns Madaktari wa CCBRT alipowatembelea kama mlezi wa Hospitali hiyo.