Wednesday, March 23, 2016

SALIM ASAS AJITOLEA KUMUUNGA MKONO RAIS DR MAGUFULI JUU YA VITA DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA ,ASAIDIA KUHUDUMIA WAATHIRIKA WA DAWA ZA KULEVYA


SALIM ASAS AJITOLEA KUMUUNGA MKONO RAIS DR MAGUFULI JUU YA VITA DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA ,ASAIDIA KUHUDUMIA WAATHIRIKA WA DAWA ZA KULEVYA
Baadhi ya  vijana  waliokuwa  wakitumia dawa  za  kulevya kwa  sasa  wameacha nazo katika Iringa Sober House
Mlezi  wa kituo  hicho  cha Iringa Sober House Bw. Godwin Msillu  (kushoto)  akiwa na baadhi ya  vijana  waliokuwa  watumiaji wa dawa za kulevya ambao  wanaishi  kituoni hapo 
Shadrack John ambae ni  mdu anaeishi  katika kituo  cha Iringa  Sober House aliyetoka  mkoa  wa Arusha  akijisomea Biblia baada  ya  kuachana na matumizi ya  dawa  za kulevya 

Na Francis Godwin, Iringa
KAMANDA  wa  umoja  wa  vijana  wa chama  cha mapinduzi (UVCCM)  mkoa  wa  Iringa Bw Salim Asas  ameunga  mkono  kwa vitendo mapambano ya vita  dhidi ya madawa ya  kulevya  nchini  yaliyoanzishwa na  Rais Dr  John Pombe Joseph Magufuli kwa kusaidia  uanzishwaji  wa   kituo  cha kusaidia waathirika  wa madawa ya  kulevya  mkoani hapa.
Bw.   Asas  ambaye  wakati  wa kampeni   za uchaguzi  mkuu alipata  kuweka bayana  mkakati  wake  wa kusaidia vijana   walioathiriwa na matumizi ya madawa  ya  kulevya  ameungana na  kituo  cha Iringa Sober  House  kilichopo Semtema  katika Manispaa ya  Iringa  kuwasaidia  vijana  hao ambao  afya  zao zimeathiriwa na madawa ya  kulevya kwa kuwakusanya na  kuwapatia  tiba.
Akizungumza na mtandao  wa matukiodaima leo   Dr Alli Ngalla ambae ni  Mkurugenzi  wa NGOs  ya Foundation for Elleviation of drug Addiction andsufferings (FADAS) wameanzisha kituo cha  kutoa  huduma kwa waathirika wa madawa ya  kulevya  cha  Iringa Sober House ambacho  kimeanza  kufanya kazi chini ya  ufadhili mkubwa  wa Bw  Asas.
Alisema  kuwa kituo  kituo  hicho   toka  kimefunguliwa  kina  zaidi ya  mwezi mmoja  ambapo  jumla ya  wategemezi 7 ambao  wanahudumiwa katika  kituo  hicho pamoja na  wasimamizi  watatu ambao pia  walikuwa ni  watumiaji wa dawa  za kulevya ambao kwa sasa  waliacha.
" Kwa  kweli  kuendelea  kwa  kituo  hiki  kumechangiwa kwa karibu na Salim Asas ambae amekuwa bega kwa  bega  kuona  vijana  walioathirika na madawa ya kulevya    wanasaidiwa na anachofanya  salim pia ni  kumuunga mkono Rais Dr Magufuli  ambae ametangaza  vita   dhidi ya madawa ya  kulevya ......hivyo bado  tunaomba   wadau  wengine   kujitokeza  kusaidia mapambano haya  ya  kunusuru afya  za  vijana  wetu "alisema Dr Ngalla.
Kuwa  lengo la  kituo  kuweza  kuwahudumia   waathirika  wa madawa ya  kulevya  kutoka  mikoa mbali mbali nchini hasa  wamelenga  kuwafikia vijana wa mkoa  wa Mbeya, Njombe , Ruvuma na Iringa japo  tafiti zinaonyesha  mkoa  wa Mbeya  ndio  unaongoza kwa matumizi ya madawa ya  kulevya.
Msimamizi  wa  kituo   hicho Bw Godwin Msillu alisema  kuwa mkakati  wa  kuanzisha  kituo   hicho  ulitokana na  mkakati  wa NGOS  ya  FADAS ambao  walikuja na mpango  wa kuanzisha kituo hicho.
Alisema  kuwa kati ya  waathirika  wa dawa za kulevya ambao  wapo  kituoni  hapo  baadhi yao ni kutoka  mkoa  wa Arusha na  kuwa  kumekuwepo  na mafanikio makubwa kwa  walengwa hao afya  zao  kuanza  kuimarika na  hivyo  kuwataka   vijana  wengine  walioathirika  na  dawa  za  kulevya  kutosita  kufika   kituoni hapo  ili  kusaidiwa zaidi.
Akizungumza  kwa niaba  ya  wenzake walioathirika na madawa ya kulevya Bw  Shadrack John alisema  kuwa amepata  kufika  mkoani Arusha  kuja  kupatiwa  huduma  hiyo  na kuwa kwa sasa hali  yake  inaendelea  vizuri  zaidi.
Huku kijana  Ibrahim Abdu alisema kuwa amekuwa akitumia madawa hayo kwa   zaidi ya miaka  10  sasa kabla ya  kuamua  kuacha na  kujiunga na  kituo  hicho   hivyo  kupongeza  jitihada za Asas  kuunga mkono  kituo   hicho huku  akiwataka vijana  wenzake  kuachana na matumizi  ya madawa ya  kulevya .