Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Serikali za Mitaa (LAAC) imesema suala la Shirika la Usafiri Mkoa Dar es Salaam (UDA) wameliweka pembeni kutokana na baadhi ya wajumbe kubadilishwa katika kamati hiyo ikiwa ni pamoja na unyeti wa suala hilo kwa masilahi mapana ya wananchi wa jiji la Dar es Salaam.
Akizungumza leo Kaimu Makamu Mwenyekiti wa LAAC , Abdallah Chikota amesema kuwa wajumbe wapya lazima wasome taarifa ya shirika hilo , ili waje na ushauri ambao utasaidia kumaliza suala hilo.
Amesema kuwa kamati itafanya kila jitihada za kukutana na jiji katika kuweza kushughulikia masuala mawili ambayo ni UDA pamoja na Kiwanda cha Nyama yamekuwa yakileta matatizo kwa wananchi ya sitofahamu.
Aidha amesema kuwa suala hilo kuwa suala la wa UDA linatakiwa kila taarifa kutoka wadau mbalimbali ziweze kupitiwa katika kuweza kuepuka kufunguliwa kesi zisizo kuwa msingi.
Chikota ametaka Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam irudishe ardhi ya kiwanda cha Nyama (Tanganyika Packers) katika mamlaka yake huku huku wakisubiri hatima ya kiwanda hicho.
Waziri wa nchi ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene amesema kuwa wanakubaliana na kamati kutokana na unyeti wa suala la Uda kwa masilahi mapana kwa wananchi.
Simbachawene amesema wamechoshwa na suala la uda na Kiwanda cha nyama na kuahidi akipata muda atakutana na wadau ili kuondokana mlolongo wa kesi zitakazotokana na ufumbuzi wa UDA na ufumkwa minajili ya kulinda masilahi ya wananchi wa jiji la Dar es Salaam.
Nae, Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita amesema kuwa yeye ni mgeni hivyo anahitaji kupata muda wa kusoma taarifa mbalimbali juu ya hoja ya UDA pamoja na suala la kiwanda cha Nyama.