Saturday, March 19, 2016

Mkuu wa MKoa wa Morogoro afunga kikao kazi cha 11 cha maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali Mkoani Morogoro



Mkuu wa MKoa wa Morogoro afunga kikao kazi cha 11 cha maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali Mkoani Morogoro
 Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Bw.Kebwe Steven Kebwe akiongea  na maafisa habari na mawasiliano wa Serikali  wakati akifunga kikao kazi cha 11 cha maafisa hao kilichofanyika mkoani Morogoro.
 Katibu mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Prof.Elisante Ole Gabriel akiongea na maafisa Habari na mawasiliano wa Serikali na kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Bw.Kebwe Steven Kebwe(wa tatu kutoka kulia) kufunga kikao cha 11 cha maafisa hao kilichofanyika Mkoani Morogoro.Wengine pichani  ni Mwenyekiti  mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO Bw.Assah Mwambene(wa kwanza kulia),Kaimu mkurugenzi wa mawasiliano ikulu Bw.Gerson Msigwa(wa kwanza kushoto) na Mwenyekiti wa chama cha maafisa Habari na mawasiliano wa Serikali(TAGCO) Bw.Innocent Mungi.(wa pili kulia).
 Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali wakimsikiliza mkuu wa mkoa wa Morogoro Bw.Kebwe Steven Kebwe wakati alipokuwa akifunga kikao cha 11 cha maafisa hao mkoani Morogoro.
Maafisa Habari na Mawasiliano wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa Mkoa wa Morogoro Bw,Kebwe Steven Kebwe(wane kutoka kushoto waliokaa) mara baada ya kumaliza kikao kazi mkoani Morogoro.