Saturday, March 19, 2016

MHE. MAKONDA AWATAKA WAMILIKI WA SILAHA KUJISAJILI UPYA


MHE. MAKONDA AWATAKA WAMILIKI WA SILAHA KUJISAJILI UPYA
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewataka wamiliki wote wa silaha jijini hapa kuwasilisha taarifa ya uhalali wa silaha zao na kusajiliwa upya kwa wakuu wa polisi wa Wilaya (OCD). 

 Aidha amewataka watu wote wanao miliki silaha hizo kinyume cha sheria kuzisalimisha kabla ya kuanza kwa Oparesheni ya ukaguzi jijini hapa Julai mosi mwaka huu. Akizungumza Dar es Salaam jana wakati alipotembelea katika Kanda Maalum jijini hapa, Makonda ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama jijini hapa, wamiliki hao wafike katika ofisi za wakuu wa polisi wa wilaya kuanzia April mosi mwaka huu hadi julai mosi mwaka huu itakapo anza oparesheni hiyo. 

Alisema lengo la hatua hiyo ni kujihakikisha na kujua idadi ya silaha zinazotumika na kuzisajili upya. "Hivyo kwa yule ambaye hakutumia siku hizo katika kuwasilisha taarifa au kusalimisha silaha tutaona kwamba anatumia silaha hiyo kinyume na kile ambacho kilikusudiwa kwa utoaji wa silaha," alisema. 

 Hata hivyo alisema kwa wale ambao hawana nyaraka nao katika kipindihicho wasalimishe silaha hizo na kwamba mtu huyo hata chukuliwa hatua na kwamba silaha hiyo itachukuliwa na kuwekwa kwenye utaratibu unaostahili. 

 Alisema lengo la kufanya hivyo ni kuhakikisha Dar es Salaam inakuwa jiji linaloongoza kwa utulivu pamoja na kusitisha matukio ya ujambazi ya kutumia silaha, au pikipiki wala kusikia milio ya silaha na badala yake ni kuona jiji lina kuwa la amani na utulivu. 

 Makonda alitumia nafasi hiyo kulipongeza jeshi hilo na kuwatangazia utaratibu mpya wa kutoa tuzo kwa askari watakao pambana na ujambazi jijini hapa ambao wanawafanya watanzania wanaishi na hosfu katika kila kipindi cha miezi mitatu. 

 Alisema hatua hiyo ambapo skari bora atakao fanya vizuri katika pambana na ujambazi watapewa sh.milioni moja na mkuu wa mkoa huo ikiwa ni shemeu ya motisha na kuwatia moya katika kutimiza majukumu yao na katika hatua ya kupambana na ujambazi.  

"Askari wanafanya kazi katika mazingira magumu katika kupambana na uhalifu hivyo kama mkuu wao wa mkoa hawezi kukaa kimya na kuona ni vyema kuweka fumo huo wa kuwaongezea motisha kwani hiyo ni kazi ngumu inayohitaji kutiwa moyo licha ya kwamba ni sehemu ya majukumu yao," alisema. 

 Kwa upande wake Kamanda Kanda Maalum Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro alisema kuna kila sababu ya kuhakiki silaha zote kwani matukio mengi yanayofanyika wakikamatwa watuhumiwa wanakutwa na silaha zinazokamatwa ni zile ambazo zilitolewa kwa umiliki kwa lengo zuri lakini inakuwa tofauti. 

 Hivyo baada ya miezi mitatu tutaanza oparesheni kubwa ya kuwakamata kwani tunataarifa za watu wote wanaomiliki silaha na kuwaomba Watanzania kujitokeza na si kusubiri kukamatwa lakini kama anaamini anatumia silaha hiyo inatumiwa kihalali ni vema kuiwasilisha na taarifa zake.

 "Hivyo ni vema kuziwasilisha kwani hakuna haja ya kusubiri kukamatwa kwani mwishowake ni kufikisha mahakamani hivyo ni bora wafike katika sehemu elekezi kwaajili kuwasilisha taarifa zao na matumizi na kama umetumia risasi kumi ueleze katika hali gani," alisema.