BALOZI                wa Uturuki nchini Yesemin Eralp amezindua kampuni mpya ya                huduma za tiketi za ndege pamoja na Utalii ya SkyPalm                Travel and Tour Ltd.
        Tukio                hilo lilitokea jumamosi hii hapa jijini ambapo balozi huyo                alitoa wito kwa wawekezaji zaidi kujitokeza kuwekeza                kwenye sekta hiyo.
        Alisema                kuwa Tanzania imekuwa ikifanya vema kwenye sekta ya utalii                huku ikiwa na vivutio vingi vya utalii vinavyovutia zaidi                na kuwavutia watalii kutokea nchi mbalimbali. Aliongeza                kuwa wageni kutokea nchi mbalimbali duniani wanahitaji                huduma kutokea kwa kampuni bora zaidi itakayowahudumia kwa                ufanisi na umakini.
        Kwa                upande wake Mkuu wa Biashara wa kampuni hiyo Meysun                Buyuksarac alisema kuwa kampuni hiyo imelenga kuimarisha                utoaji bora wa huduma za usafiri wa ndege pamoja na utalii                nchini.
        Alisema                kuwa Tanzania inazo fursa nyingi za utalii ambapo zimekuwa                zikipelekea wageni wengi kujitokeza kuja nchini kutalii,                na hivyo kupekekea wageni kutokea nje ya kuja kwa wingi na                wao kama kampuni wamejipanga kutoa huduma bora zaidi ili                kukidhi uhitaji.
                Balozi                wa Uturuki nchini Tanzania, Mh. Yesemin Eralp akizungumza                wakati wa hafla ya uzinduzi kampuni mpya ya huduma za                tiketi za ndege pamoja na Utalii ya SkyPalm Travel and                Tour Ltd.
        Mkuu wa Biashara wa kampuni mpya ya huduma za tiketi za ndege pamoja na Utalii ya SkyPalm Travel and Tour Ltd, Meysun Buyuksarac akizungumza katika hafla hiyo.
 
