Saturday, March 26, 2016

DAWASCO YABAINI WIZI MKUBWA WA MAJI MITAA YA TANDALE, DAR ES SALAAM


DAWASCO YABAINI WIZI MKUBWA WA MAJI MITAA YA TANDALE, DAR ES SALAAM
Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es salaam (DAWASCO) limebaini wizi mkubwa wa Maji ujulikanao kwa jina maarufuu kamaa wizi wa nyoka kwenye mitaa ya chama pamoja na Mkundunge Sinza Tandale Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza kwenye tukio hilo wakati wa operesheni maalum ya kubaini wizi wa Maji meneja wa Dawasco Magomeni Mhandisi Pascal Fumbuka amesema kuwa wamebaini wizi mkubwa wa Maji ujulikanao kwa jina la wizi wa nyoka ambapo wananchi wamejitengenezea laini za Maji kinyemela kwa kutumia mipira yakawaida na kutoa maji kutoka umbali mrefu nakuzipitisha kwenye nyumba zao au kuunganisha kwenye tenki za Maji nakuuza bila kibali kutoka Dawasco.
"Leo tumebaini wizi mkubwa wa Maji ujulikanao kama wizi wa nyoka kwenye mitaa  ya Sinza tandale ambapo wananchi wamekuwa wakijunganishia laini za Maji kwa kutumia mipira ya kawaida kutoka umbali mrefu nakupitisha kwenye maeneo ya makazi kinyemela bila kupata kibali kutoka Dawasco", alisema Fumbuka.
Pia Mhandisi Fumbuka amesema wamechukua hatua mbalimbali ikiwemo kuondoa laini zote za Maji kwa sababu za kiafya ,kutoa elimu kwa wakazi hao yakuwa hawaruusiwi kujiunganishia wenyewe bali wafike kwenye Ofisi za Dawasco kuomba huduma hiyo na waweze kuwekewa kihalali kwani kuna  ongezo  kubwa la Maji jijini hivyo hamna haja ya kuiba Maji ila pia hatua nyingine ni pamoja na kuwawekea kizimba (kioski) cha Maji ilikuwezesha wakazi hao kuendelea kupata huduma ya Maji.
"Baada ya kubaini wizi wa Maji kwenye mitaa ya Sinza Tandale tumechukua  hatua kadha ikiwemo kuondoa laini zote zilizounganishiwa kinyemela kwa sababu za kiafya kwani laini nyingine zimepita kwenye bomba za Majitaka , kutoa elimu kwa wakazi kuwa kuna ongezeko la Maji hivyo mtu yeyote anayehitaji huduma ya Maji afike kwenye  ofisi zetu za Dawasco tuweze kumuunganishia kihalali pia tumeweka kizimba cha Maji kitakacho toa huduma ya Majisafi ilikuwezesha wakazi waendelee kupata huduma ya Maji kama kawaida",alisema Fumbuka.
Kwa upande wawakazi wa Sinza Tandale akiwemo Mzee Seif Shabani Mohamed amekiri kuwepo kwa wizi mkubwa wa Maji kwenye mitaa hiyo nakusema kuwa unatokana na gharama kuwa kubwa za kuunganishiwa huduma ya Maji pamoja na ubabaishaji kuwa mkubwa  ukiomba huduma hiyo hivyo ameiomba Dawasco kupunguza gharama za kuunganishiwa Maji ilikufanya wakazi wenye kipato cha  cha chini kumudu gharama itasaidia kupunguza tatizo la wizi wa Maji kwani wananchi wengi watajiunganishia kihalali.
"Kweli mitaa mingi hapa Tandale kuna tatizo la wizi wa Maji ila inatokana na gharama kubwa ya ada ya kuunganishiwa huduma ya Maji na pia ukiomba kuunganishiwa mchakato unakuwa una ubabaishaji mrefu hivyo kufanya wananchi wenye kipato cha chini kutoweza kumudu gharama pamoja na kukata tama kutokana ubaishaji ila gharama zikipunguzwa itasaidia kupunguza tatizo la wizi wa Maji", alisema Mzee Seif.
Dawasco inaendelea kuwasihi  wakazi wote wa Jiji la Dar es salaam kuepuka kujiunganishia huduma ya Maji kinyemela  kwani operesheni ya kubaini wezi wa Maji kwenye maeneo mbalimbali ya jiji ni endelevu na pia ni agizo kutoka kwa waziri wa Maji na umwagiliaji Mh Gerson Lwenge pamoja na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh Paul Makonda  ambao waliagiza Dawasco kuwabaini wezi wa Maji   hivyo wale wote waliojiunganishia bila kibali kutoka Dawasco wajisalimishe iliwaweze kupewa kibali halali kwani hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa mtu yeyote atakayebainika akitumia huduma ya Maji kwa wizi.


Meneja wa Shirika la Majisafi na Majitaka Jijini Dar es salaam (Dawasco) Mhandisi Pascal Fumbuka akionyesha moja ya laini ya Maji iliyounganishwa kiholela (wizi wa nyoka) ambapo iliunganishiwa kwenye tenki la kuhifadhi Maji kwa ajili ya kuuza kwa wananchi kwenye eneo la mtaa wa mkundunge Sinza Tandale Jijini Dar es salaam.