Thursday, March 17, 2016

1,200 wataka SFO ichunguze upya Benki ya Standard



1,200 wataka SFO ichunguze upya Benki ya Standard

WATANZANIA 1,200 kutoka ndani na nje ya nchi wametia saini waraka maalumu wa kutaka uchunguzi ufanywe upya na Taasisi ya Kuchunguza Rushwa Kubwa ya Uingereza (SFO), ili ikibidi Tanzania isilipe mkopo huo. Mkopo huo wa dola za Marekani milioni 600 zilizokopwa benki ya Standard ya Uingereza.


Taarifa iliyotolewa na Mratibu wa utiaji saini hiyo 'Petition', Kapinga Kangoma imeeleza kuwa moja ya deni lisilokuwa la haki ni dola za Marekani milioni 600 ambalo Tanzania ilikopa kutoka Benki ya Standard ya Uingereza kupitia Hati Fungani.
Alisema kuwa taasisi ya SFO ya Uingereza inayoshughulika na rushwa kubwa imeonesha kuwa mkopo huu ulipatikana kwa rushwa huku Taasisi ya Corruption Watch ya Uingereza ikionesha kuwa Tanzania imepata hasara ya takribani Dola za Marekani milioni 80 (Sh bilioni 160) kwa kuchukua mkopo huu.
Alisema hata hivyo, uchunguzi wa SFO haukuhusisha maofisa wa juu wa Standard Bank makao makuu na hivyo kufunika kombe mwanaharamu apite. " Iwapo uchunguzi ungegundua kuwa Standard Bank walihusika moja kwa moja na rushwa hiyo, Tanzania ingefutiwa deni lote na kuokoa fedha nyingi sana ambazo zingewekezwa kwenye sekta za elimu, afya na maji," ilisema sehemu ya taarifa hiyo.
Alisema kuwa inatakiwa Benki ya Standard ya Uingereza ichunguzwe upya na SFO kuhusu tuhuma za rushwa ili kupatia biashara Tanzania ya Hati Fungani ya dola za Marekani milioni 600.
Imeeleza kuwa Tanzania inatarajia kuanza kulipa deni hilo kuanzia mwezi Aprili, mwaka huu wasipofanikiwa kuzuia kwa kupitia petition hiyo. Iwapo deni hili litalipwa juhudi za Rais John Magufuli kupata mapato zitaathiriwa na sekta nyeti kama elimu, afya na maji zitakosa bajeti ya kutosha.
Taarifa hiyo inasema deni la Taifa la Tanzania sasa ni Sh trilioni 30 na kutokana na ukubwa wa deni hilo, Tanzania hulipa Huduma ya Deni la Taifa takribani Sh trilioni 2.2 kila mwaka.
Hata hivyo katika madeni hayo kuna ambayo yamepatikana kwa rushwa na mengine yamechukuliwa kwa matumizi ya anasa tu. Kitaalamu madeni haya yanaitwa 'odious debts ', kama hilo la benki