Thursday, February 25, 2016

ZIARA YA NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI MIKOA YA MWANZA, GEITA NA KAGERA



ZIARA YA NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI MIKOA YA MWANZA, GEITA NA KAGERA
● Aziagiza Halmashauri kushughulikia migogoro ya ardhi .
● Azitaka kulisaidia Shirika la Nyumba ili lijenge nyumba za gharama nafuu ● Asema Halmashauri zinunue nyumba zinazojengwa na NHC kwa ajili ya watumishi wao.
● Alipongeza NHC kwa kasi ya ujenzi wa nyumba bora katika Halmashauriza Miji na Wilaya.
mab01
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Sylvester Lubala Mabula akisalimiana na Watumishi wa Hamashauri ya Mji wa Buchosa alipowasili kusikiliza na kutatua migogoro ya ardhi
MAB1
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Sylvester Lubala Mabula akipewa maelezo na mtaalam wa mifumo ya uwekaji kumbukumbu za umiliki wa ardhi alipotembelea idara ya ardhi Wilayani Misungwi. Aliyoko katikati ni Mkurugenzi wa Halmshauri hiyo Bw. Mshana. MAB2
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Sylvester Lubala Mabula na Mbunge wa Chato Mhe.Dkt Medard Kalemani wakikagua eneo la Kijiji cha Rusungwa lenye mgogoro mkubwa wa ardhi unaofanya wananchi wa kijiji hicho kukosa ardhi ya kulima na uwekaji huduma za jamii kama shule baada ya eneo la ekari 500 la kupewa mwekezaji.