Saturday, December 19, 2015

WATAOPEWA FEDHA ZA ELIMU BURE WATAKIWA KUWA NA UADILIFU NA UAMINIFU –SHIRIKISHO



WATAOPEWA FEDHA ZA ELIMU BURE WATAKIWA KUWA NA UADILIFU NA UAMINIFU –SHIRIKISHO
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

SHIRIKISHO la Wanafunzi wa Vyuo Vikuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), limesema  kuwa waliopewa wajibu wa kusimamia fedha za elimu  bure wanatakiwa uaminifu na uadilifu kutimiza suala hilo.

Akizungumza na waandishi habari  Mwenyekiti wa Shirikisho hilo, Zainabu Abdallah amesema kuwa kwa wale ambao watakiuka matumizi ya fedha za elimu bure, wamemtaka Rais John Pembe Magufuli  kutokuwa na huruma kwa yeyote atakayefanya urasimu usio na tija kukwamisha utekelezaji wa  ahadi ya wananchi ya kupata elimu bure.

Amesema maazimio hayo yametokana na kikao kilichofanyika hivi karibuni kilichojadili masuala mbalimbali ya serikali ya awamu ya tano na kulitathmini shirikisho na  hatimae kubaini kuwa wako nyuma ya kutokwenda na wakati.

Zainabu amesema katika kwenda na kasi wameunda kamati mbalimbali za shirikisho,amesema mosi wameanzisha dawati la mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu  katika kuondoa vikwazo vya kutopata mikopo kwa wakati.

Pili amesema kuwa wameunda kamati ya uwezeshaji ambayo itafanya kazi ya kuibua fursa za ajira katika midahalo na semina hali ambayo  itasaidia kuwafundisha wasomi juu ya kuanzisha biashara na kusimamia.

Zainabu amesema kuwa iwapo wao ni wasomi,inawapasa lazima waendane na kasi ya Rais Dk. John Pombe Magufuli kwa ajili ya fedha milioni 50 kwa vijana kuwa wabunifu wa miradi.



Aidha wakati huo huo Shirikisho hilo limeitaka serikali kufanya uhakiki wa watumishi feki kutokana na kazi wanazozifanya sio zao na kusababisha watu wenye sifa kushindwa kupata kazi ili kuweza kuwatumikia wananchi.