Thursday, December 03, 2015

TAFFA WAMFAGILIA MAGUFULI, WATAKA BANDARI KAVU ZIFUTWE



TAFFA WAMFAGILIA MAGUFULI, WATAKA BANDARI KAVU ZIFUTWE
 Rais wa Chama cha Wakala wa Forodha Tanzania (Taffa), Stephen Ngatunga (kushoto), akizungumza kuhusiana na kazi inayofanywa na serikali katika kudhibiti wizi na ukwepaji wa kodi na ushuru unaofanywa na Idara ya Forodha katika Mamlaka ya Mapato (TRA) na wafanyabiashara wasiowaadilifu wakati wa mkutano na waandishi wa habari ofsini kwake, Dar es Salaam jana. Kulia ni Naibu Rais, Edward Urio.
 Baadhi ya wanahabari wakiwa katka mkutano na viongozi wa TAFFA, jijini Dar es Salaam jana. 

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam. 
CHAMA cha Wakala wa Forodha Tanzania (Taffa), kimeitaka serikali kuzuia matumizi ya bandari kavu isipokuwa pale bandarini kunapokuwa hakuna nafasi ili kudhibiti wizi na ukwepaji wa kodi za serikali unaofanywa na wafanyabiashara kwa kushirikiana na wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato (TRA).

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana, Rais wa Taffa, Stephen Ngatunga alisema wizi na ukwepaji wa mapato ya serkali ni jambo la muda mrefu sana na serikali imeishapoteza mabilioni ya shilingi hadi hivi sasa na wizi huo unachangiwa na bandari kavu.

Alisema haoni sababu kwanini bandari hizo zisitumike pale tu kunapokuwa hakuna nafasi bandarini na badala yake sasa imekuwa jambo la kawaida makontena na mizigo mingine kuletwa bandari kavu moja kwa moja wakati hivi sasa bandari ni tupu haina msongamano wowote kama miaka ya nyuma.
 "Wizi na ukwepaji wa mapato ya serikali huanzia hapo" alisema na kuongeza kuwa wanajua njia zote ambazo zinatumika kuiba mapato ya serikali isipokuwa hawakuwa na pa kusemea kwa kuwa hata walipokuwa wakitoa taarifa mtandao huo wa uhalfu ulikuwa una mkono mrefu.

Alisema walitumia njia mbalimbali kujaribu kufikisha kwa serikali njama zilizokuwa zinatumika kuiba mapato ya serikali bila mafanikio na hivi sasa wapo tayari kwa lolote kwani mkombozi sasa amepatikana ambaye ni Rais John Magufuli.

"Kutokana na kasi ya utendaji wa viongozi wapya, matuko yaliyojitokeza katika idara ya frodha ya Mamlaka ya Mapati (TRA) tukiwa wadau wakuu, baadhi ya wanachama wetu wameguswa kwa njia moja au nyingine ndo maana tunaongea leo" aisema.

Alibainisha kipindi kirefu waipigia kelele hali hiyo lakini hawakusikiizwa na wizi unafanywa na kundi la watu wachache ambao hawafiki hata 10 ambao walikuwa wamehodhi biashara ya kuingiza na kutoa mizigo bandarini huku wakimiliki bandari kavu katika maenero mbalimbali jijini ambazo wanazitumia sivyo.

Naibu Rais wa Taffa, Edward Urio alisema chama chao hakitakuwa na huruma kwa wakala ambaye amehusika au atakayekamatwa akihusishwa na wizi na ukwepaji kodi unaoibuliwa hivi sasa na akibainika watamfukuza katika chama na picha, jina lake na la kampuni vitachapishwa katka vyombo vya habari iwe fundisho kwa wengine.