Thursday, December 03, 2015

MKUU WA WILAYA YA SHINYANGA AFANYA ZIARA SOKO KUU SHINYANGA.



MKUU WA WILAYA YA SHINYANGA AFANYA ZIARA SOKO KUU SHINYANGA.
Desemba 02,2015- Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro ameendelea na ziara za kushtukiza kwenye maeneo ambayo ni kero katika wilaya hiyo.Ilikuwa majira ya saa tano asubuhi,mkuu huyo wa wilaya akaabukia katika soko kuu la manispaa ya Shinyanga lililojengwa kabla ya uhuru wa Tanganyika..Ikawa faraja kwa Wafanyabiashara wa soko hilo waliodai kwa kipindi kirefu wamekuwa wakiilalamikia halmashauri ya manispaa kutokana na kushindwa kulifanyia ukarabati soko hilo.Akiwa katika soko hilo Josephine Matiro amesikiliza kero nyingi kutoka kwa wafanyabiashara hao ikiwemo ukosefu wa mitaro,kalo la maji,uchafu sokoni.Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde alikuwepo eneo la tukio..Anatusimulia kwa picha 40 kilichojiri mwanzo hado mwisho..Tazama hapa chini

Mkuu wa wilaya ya Shinyang Josephine Matiro akiwa na mwenyekiti wa soko kuu mjini Shinyanga Alex Stephen ambaye alisema kwa muda mrefu kumekuwa na kero ikiwemo ukosefu wa mitalo ya kupitishia maji machafu,kalo la maji machafu kujaa,ghuba la taka kujaa mara kwa mara.Alisema licha ya kwamba wataalamu wa halmashauri walishafanya tathmini ya namna ya kujenga mitaro lakini hakuna utekelezaji uliofanyika huku wao wakiendelea kupata kero wakati wanalipa ushuru na michango mingine inayohitajika. 

Ndani ya soko kuu la manispaa ya Shinyanga viazi vikiwa chini pembeni maji machafu
Hili ni soko la manispaa ya Shinyanga/mkoa wa Shinyanga lililojengwa zaidi ya miaka 50 iliyopita
Ndani ya soko kuu mjini Shinyanga
Afisa Masoko wa manispaa ya Shinyanga Mabina Sang'udi (wa pili kutoka kushoto) akitoa maelezo namna wafanyabishara wanavyokiuka taratibu za sokoni na kufanya soko lionekane halifai
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwa ndani ya soko kuu mjini Shinyanga,pichani juu kulia ni viatu ambavyo kimsingi havipaswi kuuzwa katika soko hilo ambalo ni maalum kwa bidhaa zinazotoka shambani tu
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiangalia ghuba la taka katika soko hilo
Uchafu katika ghuba la soko kuu mjini Shinyanga,wazoa uchafu wakitumia nyenzo duni
Mkuu wa wilaya alifika pia katika choo cha soko hilo kinacholalamikiwa kutokuwa kisafi ingawa mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Lewis Kalinjuna amedai ni kisafi na kuupongeza uongozi wa soko hilo.Hata hivyo wafanyabiashara hao walisema kumekuwa na bei tofauti tofauti ukitaka kujisaidia wakati mwingine unatozwa shilingi 200,300 au 100.
Moja ya matundu ya vyoo katika soko hilo.Kwa mujibu wa afisa biashara wa manispaa ya Shinyanga Sande Deogratius bei ya kujisaidia katika vyoo hivyo ni shilingi 300/= kwa haja kubwa,haja ndogo shilingi 200/=
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga akitoka kukagua choo ,kulia kwake ni afisa mtendaji wa kata ya Shinyanga mjini Mathias Masalu.
Mfanyabishara akiuza dagaa na makopo,ndoo tupu ndani ya soko
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro na mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Lewis Kalinjuna wakiangalia mifuko yenye chupa na makopo ndani ya soko la bidhaa za mashambani,ambapo waliagiza mifuko,maboksi,chupa na vingine vyote visivyotakiwa kuondolewa sokoni
Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Lewis Kalinjuna(mwenye nguo nyeusi) akitoa maelekezo kwa afisa masoko wa manispaa ya Shinyanga kuhakikisha kuwa kero za soko hilo zinatatuliwa haraka iwezekanavyo

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwa katika eneo la kalo la maji machafu(kulia) lililojaa na kufunikwa maboksi hali ambayo ni hatari kwa afya za wafanya biashara wa soko hilo.Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyang Lewis Kalinjuna aliahidi kukarabati kalo hilo kuanzia wiki ijayo

Afisa Masoko manispaa ya Shinyanga Mabina Sang'undi akisisitiza jambo kwa mkuu wa wilaya na msafara wake.
Mifuko ya makopo na chupa sokoni.
Badala ya kuuza bidhaa za shambani,sasa wanauza na chupa kabisaa.
Paa likiwa limetoboka katika chumba cha mama lishe sokoni,ambacho pia uongozi wa manispaa uliahidi kufanya ukarabati.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akitoka kwenye chumba cha mama ntilie sokoni
Mama Ntilie akipika katika eneo la wazi kutokana na kukosa nafasi sokoni hapo
Mama Lishe akieleza kero kwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga,ambapo alisema hawana eneo la kupikia matokeo yake wateja wanakimbia wakati wanalipa ushuru shilingi 300 kila siku
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga na mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga wakishangaa jinsi soko lilivyo chafu.
Mkuu pita na huku uone......
Bidhaa zikiwa sokoni
Ndani ya soko kuu mjini Shinyanga
Hapa ni nje ya soko biashara inaendelea,wenyewe wanadai hakuna sehemu ya kuuzia ndani ya soko...uongozi wa manispaa ya Shinyanga umeanza zoezi la kukamata wauza matunda wanaofanya biashara nje ya soko na barabarani na kutaka wafanyie biashara zao sokoni
Baada ya kutembelea soko hilo,mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akafanya kikao na wafanyabiashara wa soko hilo,alimuagiza afisa masoko wa manispaa hiyo Mabina Sang'udi kuhakikisha uchafu wote ambao uko ndani ya maboksi pamoja na chupa tupu kuondolewa ili soko liwe katika mpangilio mzuri tofauti na hali ilivyo sasa hakuna mpangilio mzuri. 
Askari polisi wakiwa eneo la tukio
Mkutano unaendelea
Mfanyabiashara Isack Ngolita akizungumzia kero katika soko hilo ambapo alisema soko hilo halina mpangilio mzuri kutokana na kutotenganishwa sehemu za kuuzia bidhaa zao
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro,mkurugenzi wa mamispaa ya Shinyanga Lewis Kalinjuna wakisikiliza kero za wafanyabiashara sokoni
Afisa afya wa manispaa ya Shinyanga Heri Nakuzelwa akizungumza.
Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Lewis Kalinjuna akizungumza katika kikao hicho.
Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Lewis Kalinjuna alisema uboreshaji wa soko hilo utaanza kutekelezwa haraka ikiwamo kujenga upya shimo la maji machafu ambalo litawekewa chujio ,kuweka mpangilio mzuri na kuanza ujenzi wa mitaro ili maji yaweze kutiririka na kuondoa kero kwa wafanyabiashara.